25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Shule mpya za sekondari Dar kuwekwa lift

Na Norah Damian, Mtanzania Digital

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ina mpango wa kujenga lift katika shule mpya za sekondari kuwezesha watoto wenye ulemavu kusoma bila vikwazo.

Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu unasisitiza nchi wanachama kuweka mifumo rafiki inayowezesha mahitaji muhimu kwa jamii hiyo.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Ofisa Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mwalimu Mussa Ally, alisema kwa kuanzia lift itawekwa katika Shule ya Sekondari Liwiti iliyopo Kata ya Liwiti ambayo ujenzi wake unaendelea.

“Malengo yetu ni kuweka miundombinu rafiki itakayowawezesha wanafunzi wenye ulemavu wanasoma bila vikwazo.  Tunajenga lift kulingana na maelekezo ya sasa, tumeanza na Liwiti tunajenga ya mfano halafu tukiona tija yake tutakwenda kwenye shule nyingine.

“Tunataka kujenga maghorofa katika Shule ya Sekondari Minazi Mirefu, Mnazi Mmoja, Kipunguni na Liwiti yenyewe,” amesema Mwalimu Ally.

Kwa mujibu wa ofisa huyo ujenzi wa shule hiyo ambayo itakayokuwa na ghorofa tano unagharimu Sh billioni 1.4 na kwamba wanatarajia Januari 2023 ianze kuchukua wanafunzi wa kidato cha kwanza.

Naye Diwani wa Kata ya Liwiti, Alice Mwangomo, amesema ujenzi wa shule hiyo utawapunguzia kero watoto ambao wamekuwa wakilazimika kwenda kusoma maeneo ya mbali kutokana na kata hiyo kutokuwa na shule ya sekondari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles