24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

SHIVATIATA walia na gharama usajili dawa asili

Na Victor Makinda, Morogoro

Wito umetolewa kwa serikali kutazama upya juu ya gharama kubwa za usajili wa dawa asili.

Wito huo umetolewa mjini Morogoro jana na Katibu wa Shirikisho la Vyama vya tiba asili nchini, Othaman Shem, wakati wa maonesho ya mimea dawa kwa wadau wa tiba asili yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo, Shem, amesema kuwa gharama kubwa za usajiri wa dawa za asili imekuwa ni kikwazo kwa wataalamu wa tiba asili kuweza kuingiza dawa hizo kwenye soko la ndani na nje ya nchi.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania, Othaman Shem.

“Tiba asili zina umuhimu mkubwa na zinafanya kazi nzuri ya kutibu sawasawa na hata kuzidi tiba za kisasa. Kikwazo kikubwa kwa tiba asili kusambaa kwa wingi nchini ni gharama kubwa za usajiri wa dawa hizo ili ziweze kukubalika kwa matumizi na kuingia sokoni,” alisema Shem.

Shem amesema kuwa kusajili aina moja ya dawa ya asili ili iweze kukubalika kisheria ni Sh milioni 1.5 kiasi ambacho amekitaja kuwa ni kikubwa mno kwa wataalamu wa tiba asili kuweza kumudu.

“Ni vema serikali ikatazama upya sheria, vigezo na gharama za ujasiri wa dawa za asali. Tunao wataalamu wengi wa tiba asili ambao dawa zao zina uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa mbali mbali lakini wanakwazwa na gharama kubwa, sheria na mlolongo mrefu wa usajiri,” amesema.

Shem alitolea mfano wa sheria namba 23 ya tiba asili ya mwaka 2002, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 kuwa sio rafiki kwa wataalamu wa tiba asili kwa kuwa pamoja na vipengere vingine ambavyo sio rafiki ina kipengere kinachozuia kutangaza tiba asili jambo ambalo amelilalmikia.

 Katika hatua nyingine Shem ameishauri serikali kufanyia mrekebisho muundo wa baraza la tiba asili kwa kuwaondoa  wote ambao sio wataalamu wa tiba hizo.

“Baraza la tiba asili linaundwa na Madaktari wa tiba za kisasa, hii sio sahihi, tunatoa wito kwa serikali kufanya marekebisho wa muundo wa baraza hilo ili liundwe na wataalamu wa tiba asili..” amesema Shem.

Naye Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, anayeshughulikia taaluma, Prof Samwel Kabote, akizungumza kwenye maonesho hayo amewashauri wataalamu wa tiba asili na wadau wote nchini kuanzisha vitalu na kupanda mimea tiba ili kuepuka na uharibifu wa mazingira kwa kuvuna mimea hiyo kwenye misitu  ya asili au misitu ya hifadhi.

“Kadri miaka inavyokwenda miti ya mimea tiba inakwisha, hivyo ni vyema wadau wa dawa za asili wakaanza kufirikia kuanzaisha vitalu vya mimea tiba kwa ajili ya kuifanya mimea hiyo kuwa endelevu,” amesema.

Aidha, Prof. Kabote alisema kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ina kitengo maalum kwa ajili ya utafiti wa mimea tiba na kinatoa ushauri kwa wadau wanaotaka kuanzisha vitalu vya mimea tiba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles