26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 5, 2024

Contact us: [email protected]

Shirika la Ndege Kenya latangaza hasara

Mbuvi Ngunze
Mbuvi Ngunze

NAIROBI, KENYA

SHIRIKA la Ndege Kenya (KQ) lilitangaza jana kupata hasara ya  Sh bilioni 4.7 za Kenya katika kipindi cha miezi sita kilichomalizika Septemba 30, 2016.

Hasara hiyo, hata hivyo imepungua ikilinganishwa na ile ya Sh bilioni 11.9 iliyopata katika kipindi sawa na hicho mwaka 2015.

Hiyo inamaanisha kuwa kampuni hiyo ilipunguza pengo la hasara kwa asilimia 60.

Kupungua kwa hasara kulichangiwa na ongezeko la abiria waliotumia ndege za shirika hilo hadi milioni 2.2.

Idadi ya abiria iliongezeka kwa asilimia nne, ambao ni sawa  na abiria 89,000 ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka jana.

Mapato yaliyotokana na usafirishaji wa mizigo yalipungua kwa asilimia 20.

Kwa ujumla, mapato ya KQ yalipungua kwa asilimia 3.5 hadi Sh bilioni 54.7 kutoka Sh bilioni 56.7 mwaka jana.

Kwa mujibu wa ripoti, ndege za KQ ziliongeza muda wa kuhudumu kwa asilimia tisa ikilinganishwa na mwaka jana.

Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya mapato ya shirika hilo jijini hapa, Mkurugenzi wa KQ, Mbuvi Ngunze, alisema kuwa kudorora kwa sarafu katika mataifa mbalimbali ya Afrika, ushindani na mabadiliko katika mazingira ya biashara ni miongoni mwa changamoto zilizochangia hasara hiyo.

“KQ limekuwa likijaribu kila liwezavyo kukabiliana na changamoto hizo ili kuboresha mapato,” alisema Ngunze alielezea wasiwasi wake kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2017, kudorora kwa sarafu ya kenya, ugaidi huenda vikaathiri zaidi mapato ya shirika hilo mwaka ujao.

Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, KQ lilipokea mkopo wa Sh bilioni 9.8 bilioni kutoka kwa serikali.

“Kampeni inayojulikana kama ‘Operation Pride” inayolenga kuboresha mapato ya kampuni itakuwa ya manufaa makubwa kwa KQ. Kampeni hiyo iliidhinishwa na serikali pamoja na wadau wengineo wa KQ,” alisema.

Alisema kuwa shirika hilo mwaka huu linalenga kuzindua ndege mpya 30 ambazo zitatoa huduma za usafiri barani Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles