26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Shigela awataka vijana kuchangamkia fursa mradi wa mbogamboga

Na Ashura Kazinja, Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigela amewataka vijana wa mkoa huo na maeneo jirani kujitokeza kujiunga katika mradi wa vijana unaoitwa Kizimba Business Model, uliojikita kwenye kilimo cha bustani na mbogamboga.

Shigela ametoa rai hiyo hivi karibuni mjini Morogoro wakati alipotembelea shamba hilo lililopo Wami Luhindo wilayani Mvomero, lililoanzishwa na Ushirika wa Wajasiliamali waliohitimu Chuo Kikuu cha Sokoine (Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative – SUGECO) kwa lengo la kuwajengea vijana kushiriki kujenga uchumi wao na Taifa kupitia kilimo.

Amesema, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa   na Rais Samia Suluhu Hassan, imejikita katika uzalishaji, ambapo mashirika ya UNDP pamoja na baadhi ya taasisi za kibenki hapa nchini zipo tayari kusaidiaa kutekeleza dhamira hiyo.

 Amewataka vijana kuitikia wito wa kufanya kazi kwa bidii kwenye mradi huo ili kujiongezea tija.

“Vijana ambao mmedhamiria kuja hapa kwenye shamba hili kwa lengo la kuzalisha mazao ya kilimo, mnapaswa kuweka jitihada kwa kuelekeza nguvu kubwa katika uzalishaji wa mazao ya kilimo,”amesema Shigela.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la  Maenedeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini  Chritina Musisi, amesema shirika hilo limefurahishwa na mradi huo na wako tayari kushirikiana katika kuwasaidia vijana kushiriki kwa kuwapatia fedha za kutoshereza mahitaji yao, kupunguza  tatizo la ajira.

Amesema vijana watakaopatikana watapelekwa katika mafunzo ya kilimo hicho nchini Israel na baada ya kipindi cha miezi 11 watarudi hapa nchini na kuanza kazi ya kulima mazao ya mbogamboga.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mariam Okash, ameshukuru shirika la  SUGECO kuwapelekea mradi huo wilayani kwake, kwani mradi huo unakwenda kutatua changamoto ya vijana wengi kukosa ajira na kuwataka vijana wenye sifa kuchangamkia fursa.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa SUGECO, Revocatus  Kimario, amesema lengo la  ni kuwainua vijana kiuchumi kwa kujiajiri katika kilimo hicho cha biashara na chenye uhakika wa soko.

Kimario amesema kuwa mazao yatakayolimwa ni yale ya bustani na mbogamboga ambayo tayari yamekwisha tafutiwa masoko, huku akitoa wito kwa halmashauri zitakazokuwa tayari kutoa ardhi zitapelekewa mradi huo ili ziweze kuongeza mapato.

Akizungumza kwa niaba ya taasisi za kibenki ambazo zimeunganishwa kwenye mradi huo, Graison Fednand ambaye ni Ofisa kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADM),  amesema  changamoto waliyokuwa wakiipata katika kutekeleza jukumu lao la kutoa mikopo kwa vijana ilikuwa ni ugumu wa kuwakusanya pamoja, hivyo shamba hilo litakuwa fursa kwao kutoa mikopo kwa vijana watakaojiunga na mradi huo.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu SUA ambaye ni Mwenyekiti wa SUGECO,  Dk. Anna Temu, amesema mradi umeanza mwaka 2011 kwa lengo la kuwawekea mazingira mazuri wahitimu wa chuo hicho na wengine wanaotaka kuwa wawekezaji wakubwa katika sekta ya kilimo kwa kuwaondolea changamoto na kutimiza ndoto zao.

Hata hivyo mradi huo unatarajiwa kuanza na vijana 500 katika utekelezaji wake ambapo vigezo vya kujiunga ni lazima vijana wawe na Stashahada au Shahada ya kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles