29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

SHAHIDI AELEZA ALIVYOMKAMATA LISSU

Na PATRICIA KIMELEMETA-DAR ES SALAAM


MKUU wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OCCID), Yustino Mgonja ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, baada ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum (ZCO), Camillus Wambura kumtaka afanye hivyo.

Huyo ni shahidi wa nne katika kesi ya kutumia lugha ya uchochezi inayomkabili Lissu aliyofunguliwa na Jamhuri.

Mgonja alieleza hayo jana   huku akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi ,mbele ya Hakimu Mkazi,Godfrey Mwambapa.

Shahidi huyo alidai kuwa Juni 28  mwaka jana,  Wambura alimpa maelekezo ya kumkamata Lissu kwa   kutoa lugha za uchochezi katika viwanja vya mahakama hiyo.

Alidai kuwa Juni 29 mwaka huo, saa 7 mchana alienda nyumbani kwa Lissu   maeneo ya Tegeta  Wilaya ya Kinondoni na kumkamata.

Alidai  baada ya kumkamata, alimfikisha katika Ofisi za ZCO na kumkabidhi.

Alidai wakati anamkamata alimwambia Lissu  kwamba alipewa amri ya kumkamata.

‘’Nilipofika nyumbani kwake nilimwambia Lissu  kuwa nimepewa amri na ZCO nikukamate hivyo kwa mamlaka hayo bila kuwa na hati ya ukamataji naweza kukukamata,” alidai  Mgonja.

Alidai  katika makosa yoyote ya jinai polisi anaruhusiwa kukamata bila kuwa na hati.

Hata hivyo aliasema kitendo cha kumpinga   Rais anapokosea siyo kosa, bali   tafsiri ya maneno aliyoyatoa ndiyo yalisababisha akamatwe na kushtakiwa kwa kutumia lugha ya uchochezi.

Katika kesi hiyo, Lissu anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu, akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alitoa kauli za uchochezi kuwa, “Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya udikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, huyu diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles