Na Upendo Mosha, Moshi
Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini imeandaa mikakati endelevu ya kuilinda benki ya Ushirika Mmoani Kilimanjaro (KCBL), hatua ambayo itasaidia wakulima kukopesheka na kukuza mitaji yao ikiwamo kuendesha kilimo chenye tija kibiashara.
Hayo yamebainishwa Julai 16, 2021 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Dk. Benson Ndiege, wakati akizungumza na Wanahisa wa benki hiyo ya ushirika kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika benki hiyo.
Amesema tume hiyo imejiwekea mikakati ya kuhakikisha inalinda benki hiyo na kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wakulima na watu binafsi kuwekeza ili kuikuza kimtaji na baadae kuwa benki ya ushirika nchini ambayo itawasaidia wakulima.
“Serikali kupitia tume hii ya maendeleo ya ushirika tumejiwekea mikakati yabkusimamia benki hii pamoja na ushirika nchini, maana wakulima wanachangamoto ya kukosa mitaji hivyo benk hii ni muhimu na ipo haja ya kuilinda na isitetereke tena,” amesema alisema Dk. Ndiege.
Aidha Dk. Ndiege amesema kwa sasa benki hiyo licha ya kupitia misukosuko mingi na kutaka kufungiwa biashara na Benki kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na kukosa mtaji, kwasasa iko vizuri kimtaji na imesimama hivyo ni vema wakulima na wanachama wa vyama vya ushirika wakachangamkia fursa ya kununua hisa.
“Benki hii iko vizuri sana na imeendelea kufanya vizuri na wanaushirika wamekubali kuendelea kuilinda kwa manufaa zaidi, kwa wale ambao watakubali kununua hisa na kuwa wawekezaji wategemee kufanya biashara nzuri,” ameongeza.
Naye Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Godfrey Ng’ura, amesema kwa sasa wanahudumia vyama vya ushirika zaidi ya 200 na kwamba imefanikiwa kuongeza mtaji kwa kushirikiana na benk ya CRDB ambapo kwa sasa mtaji wake ni zaidi ya Sh bilioni saba.
“Kwa sasa tupo vizuri hivyo nivitake vyama vyote vya msingi nchini na wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kununua hisa kwa wingi katika benki yetu ili tuweze kumiliki na kuwa na benki yetu wenyewe ambayo tutaitumia kwa fursa mbalimbali za kimaendeleo na baadae ikue na ije kuwa benk ya ushirika ya taifa.