30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yauza tani 100,000 za korosho kwa Sh bilioni 418

Na JANETH MUSHI-ARUSHA

SERIKALI imetia saini mkataba wa mauziano ya tani 100,000  za korosho zeye thamani ya Sh bilioni 418, zitakazonunuliwa na Kampuni ya Indo Power Solutions ya Kenya.

Makubaliano hayo yaliyofanyika jana jijini hapa katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC), yakishuhudiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda, Naibu Waziri wa kilimo, Innocent Bashungwa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Florense Luoga na Makatibu Wakuu kutoka wizara husika.

Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko, Hussein Mansour, Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni hiyo ya Kenya, Brian Mutembei.

Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo Bashungwa alisema korosho hizo zilizonunuliwa na Serikali kwa Sh 3,300 kwa kilo kutoka kwa wakulima baada ya agizo la Rais John Magufuli alilolitoa November 12 mwaka jana.

Alisema katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 tani 240,000 za korosho zilivuna na tayari tani 213,159 zimeshakusanywa kutoka kwa wakulima na tani 126,194 uhakiki wake umeshafanyika.

“Sasa tunauza tani 100,000 kwa Sh bilioni 418. Asilimia 95.7 ya wakulima wameshalipwa fedha zao na hadi Februari 5 wakulima wote watakuwa wamelipwa,” alisema

Naye Waziri wa Viwanda, alisema wakulima wa korosho wamelipwa Sh 3,300 kwa kilo moja ya korosho bila kukatwa kiasi chochote na kuwa wanatakiwa kumshukuru Rais Magufuli kwani uamuzi huo unawanufaisha.

Awali Prof.Kabudi alisema makubaliano hayo yaliyosainiwa yamefanyika baada ya majadiliano yaliyozingatia kanuni na Sheria.

Alisema kuwa korosho ghafi hiyo ni awamu ya kwaanza  na kuwa wataendelea kutafuta masoko ya kimataifa na kuwa malipo ya korosho hizo yatafanyika ndani ya wiki moja na kampuni hiyo kuchukua mzigo wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles