22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatakiwa na mpango kupunguza foleni Dar

jamm1Na Mwandishi Wetu, Dodoma
SERIKALI imeshauriwa kuwa na mpango wa miaka 50 hadi 100 utakaosaidia kutatua msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
Ushauri huo, umetolewa bungeni jana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika taarifa yake ya utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo katika kipindi cha kuanzia Januari 2014 hadi Januari 2015.
Akisoma taarifa hiyo, mjumbe wa kamati hiyo, Athuman Mfutakamba, alisema usanifu huo unatakiwa kuangalia ongezeko la watu katika jiji hilo kwa kuwa kila mwaka watu wanaongezeka.
“Usanifu wa mipango lazima uzingatie uwepo wa mfumo wa njia mchanganyiko, hata kama kwa kipindi hiki kuna uwezo wa kujenga miundombinu ya mabasi yaendayo kasi.
“Kwa kuzingatia jiografia ya Jiji la Dar es Salaam, mipango hii iende kwa kuzingatia mifumo ya usafiri ya mabasi yapitayo juu ya maji, usafiri wa treni chini ya ardhi maarufu kama metro na barabara za juu ziitwazo flyovers.
“Mifumo mingine ni reli za umeme aina ya trams pamoja na nguzo zake katika miundombinu ya barabara za mjini na njia nyingine yoyote ya usafiri ambayo inaweza kuwamo katika mfumo huo.
“Kwahiyo, hatua ya usanifu wa namna hii ikichukuliwa sasa, itaokoa fedha nyingi huko mbele, na pia itatoa fursa kwa Serikali kuongeza njia moja baada ya nyingine kwa kadiri fedha zitakavyopatikana,” alisema.
Alisema kamati yake, inapongeza juhudi za Serikali za kutatua msongamano katika jiji hilo, kwa kutekeleza Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi Dar es Salaam (DART).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles