Andrew Msechu, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amesema miradi mingi ya uwekezaji katika gesi inaonekana kuchelewa kutokana na sababu za kitaalamu, kwa kuwa Serikali na wawekezaji wanahitaji kujiridhisha kuhusu faida za miradi hiyo.
Dk. Kalemani amesema hayo jijini Dar es Salaam leo Jumanne Septemba 25, wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa Mafuta na Gesi jijini.
Amesema kutokana na hali hiyo, mara nyingi miradi hiyo inachelewa kutokana na sababu za wawekezaji wenyewe ambao wanataka kujiridhisha kabla hawajawekeza mabilioni yao kwa Watanzania.
“Hizi ni sababu za kitaalamu. Wakati wawekezaji wakitaka kujiridhisha kabla ya kuwekeza mabilioni yao hapa, Serikali pia huwa inahitaji kujiridhisha kwa kuhakikisha miradi hiyo inakuwa na manufaa makubwa na endelevu kwa taifa letu,” amesema.