25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yapiga marufuku uuzwaji wa samaki wachanga Kilimanjaro

Na Upendo Mosha,Mwanga

Serikali imeafiki kupiga marufuku uuzwaji wa samaki wachanga katika masoko yote ya wilaya za Mwanga, Simanjiro na Moshi Vijiji hatua ambayo itasaidia kukabiliana na kuthibiti vitendo vya uvuvi haramu katika bwawa la nyumba ya Mungu ambavyo vimeendelea kushamiri.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akizungumza na wajumbe wa Kikao cha ujirani mwema (hawapo pichani) kilichojadili kuhusu usimamizi shirikishi wa rasilimali za Uvuvi kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu ambacho kimejumuisha Viongozi na Wataalam kutoka Wizara na Halmashauri za Wilaya ya Mwanga, Moshi Vijijini na Simanjiro. Kikao kimefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Kindoroko wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro. (28.04.2021)

Aidha, serikali imedhamiria kuongeza nguvu ya kulinda bwawa hilo kwa kununua boti ya kisasa itakayosaidia kuongeza Doria na kukabiliana na wavuvi haramu ambao wamekuwa wakiharibu mazalia ya samaki.

Akizungumza Jana Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatamah,wakati wa kikao cha ujirani mwema,kilichofanyika wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro,kilichokuwa na lengo la kujadili mikakati ya kusimamia rasilimali za uvuvi Katika bwawa hilo.

Alisema uuzwaji wa samaki Katika masoko ya wilaya hizo imekuwa ni chanzo kikubwa cha kuendelea kwa vitendo vya uvuvi haramu katika bwawa la nyumba ya Mungu kutokana na kuwepo kwa wateja Katika masoko hayo.

“Wizara imekubaliana na azimio la kikao hichi cha ujirani mwema cha kupiga marufuku uuzwaji wa samaki wachanga Katika masoko ya wilaya zote tatu ambazo wametoa siku Saba na sisi tunawajibu wa kulinda bwawa letu hivyo tutatoa boti kuimarisha doria,”alisema Dk. Tamatamah.

Alisema asilimia kubwa ya uvuvi unaofanywa Kktika bwawa hilo umekuwa ni haramu na kwamba jitihada za makusudi zinapaswa kufanyika Katika kudhibiti uhalifu huo ikiwa ni pamoja na watumishi wa idara hiyo kuwa waadilifu.

Katika hatua nyingine alisema wizara hiyo ipo katika mchakato wa kuunda chombo maalumu cha ulinzi wa rasilimali za uvuvi nchini ili kukabiliana na uvuvi haramu.

“Tunaunda kikundi au kikosi chetu ambacho kitashirikisha watu mbalimbali ikiwemo polisi kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya na tutakiwezesha vifaa maalumu Kama vile boti za dori kukabiliana na changamoto hizi za uvuvi haramu katika mabwa na maziwa yetu.

“Watumishi wanapaswa kusimamia na kutekeleza sheria vizuri lakini pia wadau ambao ni wavuvi wanapaswa kutusaidia katika ulinzi shirikishi ili uvuvi uwe endelevu,”alisema.

Willium Mghuni ambaye Afisa uvuvi kituo cha kudhibiti uvuvi Kanda ya Kaskazini alisema zaidi ya asilimia 90 ya uvuvi unaofanywa katika Bwawa la Nyumba ya Mungu Ni haramu na umesababisha kuhatarisha maisha ya Askari na maafisa uvuvikushambuliwa,kujeruhiwa na wengine kupoteza maisha.

“Wananchi tunapoenda kukamata wanapiga yowe na na kukusanyika na kuanza kutushambulia tunawenzetu wamwvunjwa mikono wamejerujiwa vibaya na baadhi kupoteza maisha tunafanyakazi Katika mazingira magumu Sana uvuvi haramu unaendelea kutokana na changamoto zinazotukabili wakati wa Doria,”alisema.

Afisa uvuvi wilaya ya Mwanga, Said Msemwa alisema wavuvi haramu wengi wamekuwa wakivua samaki wachanga kwa nyavu haramu ambazo zimekuwa zikiingia nchini kwa njia za panya.

“Nyavu hizi zimekuwa zikisababisha kazi yetu kuwa ngumu kwa kuzidiwa kwani wamekuwa wakiunda umoja wao wa kusaidiana maana kila tunapokamata tunawaga faini Ila wanachangishana na kulipa,”alisema.

Naye Mkuu wa wilaya ya Mwanga, Thomas Apsoni,aliwaonya baadhi ya watumishi ambao wamekuwa wakitoa siri za mikakati ya operesheni za kukamata zana hizo haramu na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa atakayebainika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles