24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaonya Askari wanaofanya oparesheni kujinufaisha

Na Sheila Katikula, Mwanza

Serikali imekemea oparesheni zinazofanywa na baadhi ya Askari wa Uhamiaji ambazo zinawanufaisha wao kwa maslahi yao binafsi bila ridhaa ya ofisi kwani kufanya hivyo ni kosa ni vema  misako yote kufanyika kwa uwazi na usimamizi.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi yenye lengo la kuimalisha utendaji kazi wa majeshi hayo pamoja na ushiriki wa wananchi katika ulinzi shirikishi.

Simbachawene alisema baadhi ya maafisa hufanya misako kwa masilahi yao binafsi  kwani ni vizuri ifanyike kwa uwazi , usimamizi  na kupewa kibali kutoka kwenye ofisi hii ni kwa sababu ya kuepuka  askari ambao siyo waaminifu.

“Mnafanya kazi vizuri sana na ninawapongeza,lakini kuna baadhi yenu wanafanya oparesheni za kimya kimya bila kupewa amri na ofisi na wanafanya misako kwa maslahi yao binafsi sasa watambue tumeishawabaini na muda si mrefu wataumbuka,” alisema Simbachawene.

Aidha, Simbachawene amemtaka Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Bahati Mwaifuge kuhakikisha anafanya misako sehemu mbalimbali ikiwamo machimboni, kwa wavuvi na kanda ya ziwa ambapo kuna mwingiliano wa watu wengi  ambao baadhi yao siyo wazuri hupora ajira na kupelekea watanzania kukosa ajira kwenye nchi yao.

Kwa upande wake Mwaifuge alisema wanakabiliwa na changamoto ya watumishi ambayo inayosababisha ugumu wa kazi huku akitolea mfano wilaya ya Ukerewe kuna visiwa 38 lakini kuna askari wa uhamiaji wawili.

“Tunakabiliwa na uhaba wa magari  yaliyopo ni chakavu lakini tunafanya kazi hivyo hivyo,wilaya ya Sengerema ina gari chakavu lakini tunalitumia  na kwenye wilaya nyingine tunatumia pikipiki  Kwani hivi sasa kesi zote zinafanyikia huko huko tunatuma  wanasheria na askari wanaenda huko.

“Mkoa mzima  tunajumla ya watumishi 71,wakiwemo raia wanne,maaskari 33, maafisa 10 na wakaguzi 24 japo  kuna upungufu lakini tunafanya kazi hivyo hivyo na tulifanikiwa kumkamata kinala wa usafirisha wa wahamiaji haramu na kesi yake bado inaendelea,”alisema Mwaifuge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles