26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kuwabana waajiri

Ramadhani Hassan na Pendo Mangala
WAFANYAKAZI Mkoa wa Dodoma wameishauri Serikali ihakikishe waajiri wanawaongezea mishahara kwa sababu malipo wanayolipwa sasa ni madogo.
Hayo yalisemwa jana na Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Mkoa wa Dodoma, Ramadhani Mwenda, wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Mwenda alisema kipato cha ujira wa mshahara wa mwezi hakitoshi na kwamba mishahara ya watumishi ni midogo inayolingana na posho ya kikao kimoja cha baadhi ya viongozi wa Serikali.

“Kipato cha ujira wa mshahara kwa mwezi tunacholipwa wafanyakazi hakiridhishi kabisa kwa sababu ni sawa na posho ya siku moja ya kikao cha baadhi ya viongozi wa Serikali na Taasisi zake.
“Malipo haya kidogo athari zake ni kukosekana kwa tija mahala pa kazi kwani wafanyakazi hutumia kujikumu kwa siku saba, tunaomba tupandishiwe hadi ifike 315,000 kwa mwezi,” alisema Mwenda.
Alisema upungufu katika sheria za kazi unatoa mwanya kwa baadhi ya wawekezaji kuwa mabingwa wa kukwepa fidia, kulipa kodi ya mapato na ushuru hivyo taifa kutonufaika na uwekezaji wao.
Aidha, Mwenda alisema yapo madeni mengi sugu ya wafanyakazi yanayotokana na malimbikizo ya madai mbalimbali halali kama likizo, uhamisho, matibabu, gharama za kujisomesha ambayo yamekwama kwa visingizio mbalimbali.
Mwenda pia alilalamikia makato makubwa ya kodi kwa wafanyakazi pamoja na uonevu wanaofanyiwa wafanyakazi sehemu za kazi huku Serikali ikifumbia macho maombi ya kupunguzwa kodi kwa wafanyakazi.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa, aliwataka wafanyakazi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili washiriki kwenye uchaguzi ambao utawezesha kupatikana kwa viongozi bora watakaopunguza kero zao za muda mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles