Na Christina Gauluhanga, Dar es Salaam
Serikali imeombwa kuzidi kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji wengi wa ndani na nje hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 29, katika mkutano ulioandaliwa na Chama wa Waajiri Tanzania (ATE), Mkurugenzi Mtendaji, Dk. Aggrey Mlimuka amesema endapo Watanzania na wawekezaji wageni watawekeza biashara endelevu itazidi kuchagiza kwa kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.
Amesema uwekezaji wa China ni mkubwa na wenye tija kwa Tanzania kwa sababu unaongeza ajira na viwanda hapa nchini.
“Uhusiano wa China na Tanzania ni wa muda mrefu hivyo ni vyema kuendelea kuweka Mazingira ya uwekezaji ili kuwavutia zaidi Kibiashara,”amesema Mlimuka.
Katika mkutano huo ulioandaliwa na ATE umeshirikisha wawekezaji toka nchini Norway na China.