27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Serikali yamfungia Diamond ndani, nje

ADAM MKWEPU – DAR ES SALAAM

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), limewafungia wanamuziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’ na Raymond Mwakyusa, kufanya onyesho lolote ndani na nje ya nchi kwa muda usiojulikana pamoja na kukifuta kibali cha tamasha la ‘Wasafi Festival 2018’.

Baraza hilo lilifikia uamuzi huo baada ya kugundua kuwa wasanii hao walikuwa wakidharau uamuzi uliotolewa na baraza hilo kwa kuendelea kuuimba wimbo wa ‘Mwanza’ ambao ulikuwa umefungiwa.

Novemba 12 mwaka huu, Basata liliamua kuufungia wimbo huo kwa madai ya kuwa na mistari iliyokuwa ikikiuka maadili katika jamii.

Taarifa ya Basata iliyotolewa jana ilieleza kuwa mbali ya kuwafungia wasanii hao, pia wamesitisha kibali cha tamasha la ‘WasafiFestival 2018’ baada ya kukiuka sheria za uendeshaji.

“Baraza limefikia uamuzi huu kwa sababu ya wasani ihawa kuendelea kuonyesha dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia masuala ya sanaa nchini.

“Pia kumekuwa na uvunjifu wa maadili uliokithiri unaofanywa na waandaaji wa tamasha la ‘Wasafi Festival’, chini ya uongozi wake, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’.

“Pamoja na maelezo hayo baraza linatoa taarifa kuwa kibali cha tamasha la ‘Wasafi Festival 2018’ kimesitishwa kutokana na ukiukwaji wa sheria, taratibu na uendeshaji wa tamasha hilo hapa nchini,” ilisema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles