26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHA CHAI MPONDE

NA AMINA OMARY- BUMBULI

SERIKALI imemaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya wakulima wa chai wa wilaya za Lushoto na Korogwe na kampuni ya Mponde Tea Estate uliosababisha kufungwa kwa kiwanda cha chai cha Mponde baada ya kuagiza kiwanda hicho kianze kazi.

Uamuzi huo wa Serikali umetangazwa leo Alhamisi Novemba Mosi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kweminyasa kata ya Mponde, wilayani Lushoto ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya kikazi ya siku Tatu mkoani humo.

Majaliwa amesema mwaka 1999 Serikali iliamua kuwapa wakulima wa chai na kiwanda hicho  kwa ajili ya kuwawezesha kuwa na sehemu ya kuchakata chai yao lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi, Imeamua kukirudisha serikalini baada ya kuwepo migogoro iliyoathiri uzalishaji kiwandani hapo.

“Waziri Mwijage na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo hakikisheni kazi ya kukagua kiwanda na mitambo inafanyika haraka na kubaini mitambo ipi ni mizima na ipi ina hitilafu ili ukarabati ufanyike na kiwanda kianze kazi mara moja.

“Serikali imeamua kukichukua kiwanda hiki ambacho awali ilikikabidhi kwa wakulima wa chai na kwamba itahakikisha lengo lake la kuboresha kilimo linafanikiwa na  wakulima wanaendelea kulima zao la chai hatutaki kusikia masuala ya Utega wala Mponde hapa si mahali pake,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Amewasisitiza wakulima wafufue mashamba yao kwasababu sasa hivi kiwanda ni cha serikali  hivyo watakuwa wamepata sehemu ya kuhakiki   chai yao.

Aidha kuhusu suala la madeni ya watumishi, Waziri Mkuu ameagiza watafutwe na madai yaorodheshwe kwa ajili ya malipo, amewahakikisha wananchi hao kuwa suala la ajira zilizopotea baada ya kiwanda hicho kufungwa zitarudi kwa sababu Serikali inataka kuona kiwanda hicho kikifanya kazi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles