Na Sheila Katikula, Mwanza
Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema gereza na Butimba lililipo jijini hapa lina idadi kubwa ya mahabusu ni vema kutupia jicho la karibu ili kuweza kusikili mashauri ya kesi zao na haki itendeke kwa watu hao.
Hayo aliyasema jana kwenye ziara yake ya Siku moja alipotembelea gereza hilo na kuzungumza na watumishi na wafungwa alisema gereza hilo lina wafungwa zaidi ya 1000 na mahabusu 760 kasi ya siyo nzuri katika kusikiliza mashauri yaliyopo hasa kwenye mahakama kuu.
Alisema atahakikisha anazungumza na Waziri wa Katiba na sheria ili waweze kuona haki inatendeka dhidi ya wahumiwa hao.
“Nimesikiliza changamoto za mashauri kama mnavyofahamu kwenye magereza kuna watu wa mbalimbali nimeongea nao japo siyo wote ili niweze kujua mambo yao ambayo hawanahisi hawakutendewa haki nimeyachukua nitajalibu kuwasiliana na vyombo husika ili kuhakikisha wanayafanyia kazi masuala hayo ili haki itendeke,” alisema Simbachawene.
Alisema Serikali ya awamu ya sita imeanza kupunguza baadhi ya changamoto zikiwamo za kununua sare, masilshi madogo madogo na nyongeza zimeanza kutokea kwa mfano fulsa mbalimbali za kupunguza makali ya askari na mengine walitonieleza askari hawa nitayapeleka kwenye mamlaka ili tuweze kuona jinsi ya kuyapunguza,” alisema Simbachawene.
Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Butimba Mkoa Mwanza, Peter Anatory alisema gereza hilo linakaa na wahalifu asilimia 75.18 ambao wametoka sehemu mbalimbali na watumishi waliopo ni asilimia 52.12.
Hata hivyo, Anatory alimshukru Waziri huyo kwa kutembelea gereza hilo na kutoa maelezo kwa wahumiwa na mahabusu hao na kusikiliza changamoto zao.
“Nimefurahi kuona waziri akizungumza na wahalifu hawa na kuwasihi kuishi kwa amani na upendo na kuwata kutumikia sehemu ya adhabu kwa walio hukumiwa na mahabusu kuendelea kuwa watulivu ili waweze kusubili mahamuzi ya kimahakama,”alisema Anatory.