24.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaipongeza UNFPA kwa kusaidia kudhibiti ukatili wa kijinsia nchini

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga

Serikali imepongeza juhudi za Wadau wa Maendeleo nchini ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba ukatili wa kijinsia unakomeshwa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa leo Mei 23, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Mboni Mhita alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA), Melissa McNeil Barrett, kuhusu ustawi wa mtoto wa kike na mwanamke katika jitihada za kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake, wasichana na watoto.

“Sisi Serikali tunapongeza juhudi za wadau wa maendeleo hususan UNFPA na wadau wengine kwa namna ambavyo wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba ukatili kwa wanawake na watoto nchini unadhibitiwa.

“Upande wetu kama Serikali tutaendelea kutoa ushirikiano kwa UNFPA, UNWOMEN, KOICA na wadau wengine katika kuhakikisha kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na mila kandamizi dhidi ya wanawake, wasichana na watoto vinatokomezwa na kuwa historia katika jamii yetu,” amesema Mhita.

Upande wake, Melissa McNeil amesema UNFPA sambamba na wadau wengine wa maendeleo wataendelea kushirkiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na mila kandamizi dhidi ya wanawake, wasichana na watoto vinatokomezwa nchini.

Ikumbukwe kuwa UNFPA na UN WOMEN wanatekeleza mradi wa pamoja kwa Ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Korea Kusini(KOICA) mradi ambao umejikita katika kuwawezesha na kuwainua wanawake na wasichana kiuchumi na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana katika Mkoa Wa Singida Wilaya ya Ikungi na Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.

Kupitia mradi huo wa pamoja, UNFPA na UN WOMEN kwa Ufadhili wa KOICA wanatarajia kuzindua na kukabidhi rasmi Kituo cha Huduma Shufaa Kilichoko Msalala na Ofisi ya Polisi Dawati la Jinsia Wanawake na Watoto iliyopo Bugarama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles