23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yahimiza Wasanii kusajili kazi zao kwenye mamlaka husika

Na Projestus Binamungu, Dodoma

Serikali imetoa wito kwa Wasanii kuendelea kusajili kazi zao katika mamlaka zinazo husika ili zilindwe kisheria na malaka hizo katika kuhakikisha zinawanufaisha na kufanikisha ndoto zao.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa wakati akijibu maswali ya baadhi ya Wabunge waliotaka kujua msimamo wa Serikali katika kuthibiti wizi wa kazi za Sanaa kupitia ombwe kubwa la uwepo wa teknolojia zinazo wawezesha wezi kudurufu kazi za wasanii na kuziuza bila kibali cha msanii husika.

Katika kikao hicho baina ya watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii, Waziri Bashungwa amewaelezea wajumbe kuwa nia ya Serikali ni kuona vijana wananufaika kupitia kazi zao, lakini kwa kufuata Sheria za nchi, Kanuni, Taratibu na Miongozo zilizowekwa kwa lengo la kulinda masilahi yao.

“Kwa hiyo ndugu zangu wajumbe tuendelee kusaidizana kuwahimiza hawa vijana wetu kila mmoja kwa nafasi yake kwamba ni muhimu kusajili kazi zao, ili linapotokea suala la kuibiwa kazi tuwe na meno na sehemu ya kuanzia kisheria katika kufuatilia haki ya msanii husika” amesema Waziri Basungwa mbele ya kamati hiyo ya Bunge.

Awali Katibu Mkuu wa Wizira ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbasi amesema Wizara hiyo inaendelea na uratibu kuona namna bora inavyoweza kuwapeleka wataalamu wa sanaa nje ya nchi kujifunza na kuongeza ujuzi zaidi ili baadae warejee hapa nchini kuwasaidia wasanii na hasa wasanii wachanga kuzalisha kazi zenye ubora zaidi.

Akizungumza kabla ya kuhairisha kikao hicho, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii, Aloyce  Kamamba amepongeza hatua zinazo fanywa na Wizara ya Utamadunia, Sanaa na Michezo ikiwa ni pamoja na hatua ya kuwezesha kutengwa kwa asilimia tano ya mapato kutoka kwenye michezo ya kubahatisha ambayo inaiwezesha Wizara kupata fedha kiasi cha shilingi Milioni 400 kwa kila robo ya mwaka kutokana na asilimia hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles