27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yahimiza ushirikishwaji zaidi Anuani za makazi

Na Mwandishi Wetu, Pwani

Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kaspar Mmuya amehimiza Ofisi za Umma na Ofisi Binafsi kuweka anuani za makazi katika majengo ya Ofisi zao ili kuwa mfano kwa wananchi wengine.

Amesesisitiza kuwa anuani hizo zitasadia kuonesha jina la Ofisi yenyewe Mtaa iliyopo na eneo ambalo posti kodi hiyo ipo.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri  Mkuu, Kaspar Mmuya akiangalia kibao cha anuani za makazi kilichowekwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Naibu Katibu Mkuu, Mmuya amesema hayo Mei 13, 2022 katika ziara yake mkoani Pwani alipotembelea na kupokea taarifa ya Mkoa ya utekelezaji wa Anuani za makazi ambapo kwa sasa ngazi ya Taifa zoezi hilo limefikia asilimia 90 ya matarajio nakwamba mikoa kwa mikoa inazidiana katika utekelezaji wa zoezi hilo.

Mmuya ameupongeza Mkoa wa Pwani kwa kutekeleza vyema zoezi la uwekaji wa anuani za makazi na kufuata miongozo iliyowekwa katika utekelezaji wa anuani za makazi.

“Ziara imelenga kujionea uhalisia ili mwezi huu, tutumie kurekebisha dosari chache tulizogundua kwa kupokea taarifa kwenye mfumo au kwa ziara mbalimbali tunazozifanya au taarifa tunazopatiwa.

“Zoezi la anuani ya makazi ni endelevu, kila mmiliki mwenye eneo ambalo limejengwa au halijajengwa anapaswa kuwa na namba, hiyo itasaidia kujua mahali eneo lilipo, wananchi wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya umuhimu wa  zoezi la uwekaji wa anuani za makazi na itaongeza dhana ushirikishwaji wa wananchi,” amesema Naibu Katibu Mkuu Mmuya.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri  Mkuu, Kaspar Mmuya akipokea taarifa ya utekelezaji wa anuani za makazi ya Mkoa wa Pwani  kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Ramadhani Mbura, (aliyesimama) kujionea utekelezaji wa zoezi hilo.

Akihitimisha Kaimu Injinia wa Tanroad Mkoa wa Pwani, Meneja Heririsper Mollel amesema utekelezaji wa anuani za makazi umefika katika hatua nzuri ukamilishaji wake kwa sasa wamejikita katika kurekebisha vibao vilivyokosewa.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Yona Mwakilembe, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri  Mkuu, Kaspar  Mmuya mara baada ya kuwasili kwa ajili  kujionea utekelezaji wa zoezi la anuani za makazi katika Mkoa wa Pwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles