Ramadhan Hassan,Dodoma
Katika kuhakikisha Jeshi la Magereza linajitosheleza kwa chakula cha wafungwa na mahabusu Serikali imeendelea kulipatia Jeshi zana na pembejeo mbalimbali za kilimo kupitia fedha za matumizi ya kawaida.
Hayo yameelezwa leo Jumanne Mei 21 Bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Lyimo (Chadema).
Lyimo amehoji nini mkakati wa Serikali kuhakikisha Magereza zinajitegemea kwa chakula.
Akijibu swali hilo Masauni amesema katika kuhakikisha Jeshi la Magereza linajitosheleza kwa chakula cha wafungwa na mahabusu Serikali imeendelea kulipatia Jeshi zana na pembejeo mbalimbali za kilimo kupitia fedha za matumizi ya kawaida.
Masauni amesema katika bajeti ya 2018-2019-2022-2023 Serikali ilitenga fedha za miradi ya maendeleo jumla ya sh. bilioni 3 kwa ajili ya ununuzi wa zana mbalimbali za kilimo na kukamilisha miundombinu ya Gereza la Idete.