25.6 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YACHUNGUZA UTAJIRI WA KAKOBE


Na AGATHA CHARLES - Dar es Salaam

SIKU chache baada ya kiongozi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Askofu Zakaria Kakobe, kusema kuwa ana fedha nyingi kuliko Serikali, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema inamfuatilia ili kujiridhisha iwapo ana kipato hicho, vyanzo vyake na kama analipa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere, alisema licha ya Kakobe kutoa kauli hiyo, lakini hakuna kumbukumbu zake za ulipaji kodi.

“Sisi watu wa kodi tumeipokea kauli yake kwa unyenyekevu mkubwa, kwa sababu tunawapenda watu wenye fedha nyingi.

“Alisema ana fedha nyingi kuliko Serikali. Kama mtu ana fedha kuliko Serikali ambayo sisi tunajua inatoa huduma, inanunua ndege, inajenga reli ya kisasa ya standard gauge, imejenga barabara, Serikali inayotoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia dawa hospitalini, inatoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi, lakini tunaambiwa imezidiwa fedha na Askofu Kakobe, basi ni jambo jema,” alisema.

Kichere alisema baada ya kauli hiyo na kwa kuwa matajiri wanaolipa kodi wanajulikana, TRA iligundua kuwa Kokobe hayumo katika kumbukumbu za walipakodi.

“Hatuna kumbukumbu ya ulipaji kodi wake, kuna watu ambao ni matajiri, lakini hawaizidi Serikali na wamekuwa wakilipa kodi na kuonekana katika kumbukumbu zetu. Lakini tajiri Askofu Kakobe si miongoni mwao. Hivyo basi sisi watu wa kodi tunataka tujiridhishe kuhusu suala la kodi linalomhusu Askofu Kakobe na utajiri wake,” alisema.

Pia alisema kwa kuwa wao ni wataalamu wa kodi, watafahamu kuhusu kipato cha Kakobe………..

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles