27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MKEMIA MKUU: BABA WENGI WALIOPIMA DNA 2017 WATOTO SI WAO


NA AZIZA MASOUD - DAR ES SALAAM

JUMLA ya sampuli 72,000 zimepimwa na Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) katika kipindi cha Januari hadi Desemba, mwaka huu na kati ya hizo, 1,177 zilikuwa za vinasaba (DNA) ili kutambua uhalali wa wazazi kwa mtoto na majibu yalibainisha kuwa baba wengi hawakuwa halali.

Akizungumza na MTANZANIA JUMAPILI ofisini kwake juzi, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, alisema idadi ya sampuli hizo za DNA zimepatikana katika majalada 338  yaliyowasilishwa katika kipindi cha Januari hadi Desemba, mwaka huu yaliyokuwa na lengo la kufanya utambuzi wa uhalali wa baba kwa mtoto, kesi za jinai, mirathi na utambuzi wa jinsi tawala za mtoto.

“Katika upimaji wa sampuli za kutambua uhalali wa baba kwa mtoto kwa mwaka huu, baba wengi walikutwa si wazazi halali wa watoto waliokuwa wanalalamikiwa,” alisema.

Profesa Manyele alisema idadi ya sampuli hizo kwa mwaka huu zimeongezeka  ukilinganisha na mwaka jana ambazo zilikuwa 554 kati ya majalada 332.

Pia alisema ongezeko la majalada ya DNA limetokana na jamii kuhi……………………..

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles