20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaahidi kuendelea kushirikiana na wadau kunyanyua wanawake

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau ili kuhakikisha wanawake wanapata fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi na kuendeleza biashara zao.

Hayo yameelezwa Agosti 28, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima alipokuwa akizindua Programu ya kuwawezesha wanawake kiuchumi ijulikanayo kama Women Empowerment Program (WEP) inayosimamiwa na kuratibiwa na Benki ya amesema uchumi unapoimarika ndivyo familia inakuwa na ustawi bora na kupunguza madhira ya vitendo vya ukatili kwenye familia.

“Kwa takwimu tulizonazo, takriban asilimia 70 ya wanawake bado wapo kwenye ajira zisizo rasmi wakijishughulisha na biashara ndogo ndogo kama mama ntilie na kazi za nyumbani. Kwa mfano, kwa mujibu wa takwimu za Finscope za mwaka 2017, kati ya watu 3,014,106 waliokuwa kwenye ajira rasmi, wanawake walikuwa 1,107,917 sawa na asilimia 36.8 tu.” Alisema Waziri Dkt. Gwajima

“Ni matumaini yangu kuwa programu hii ya WEP ya Benki ya Exim imekuja muda muafaka na itakuwa chachu ya kupunguza pengo ili na kuwafanya wanawake washiriki kikamilifu katika sekta ya kifedha,” alisisitiza Waziri Dk. Gwajima

Katika hatua nyingine Waziri, Dk. Gwajima ameipongeza Benki ya Exim Tanzania kupitia mpango huo, kwa kutoa mkopo bila riba wa dola elfu kumi (takribani shilingi milioni 25) kwa wahitimu watatu bora kwa kipindi cha miaka mitatu na kusema jitihada hizo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Akieleza juhudi za Serikali juu ya kuwawezesha wananchi hasa wanawake kiuchumi Waziri Dk. Gwajima amesema Serikali imeanzisha jumla ya Mifuko 61 ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi na hadi sasa imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 2.22 kwa wanawake millioni 5.3 na mwaka 2018, Serikali ilipitisha sheria ambayo ilizielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba (Wanawake 4%, Vijana 4% na Watu wenye Ulemavu 2%).

“Tangu kipindi hicho, mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 63.489 imetolewa na kuwanufaisha wanawake zaidi ya 938,800,” amesema.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu amesema Benki hiyo imefanikiwa kushirikiana na wadau wengine katika kuwezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa za kupata mikopo isiyo na riba ambayo imewasaidia kupata mitaji na kuongeza vifaa vya uzalishaji hivyo kuongeza masoko kwa ajili ya bidhaa zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Ndoto Hub, Faraja Nyarandu amesema kuwa mpaka sasa kwa kushirikiana na Benki ya Exim wameweza kuwafikia wanawake 63,000 katika kuhakikisha wanawake wanapata fursa za kuendeleza ndoto za biashara zao kwa kupata mitaji na masoko ili kupata mafanikio katika biashara zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles