25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Serikali wilayani Muleba kutumia Milioni 60 kukarabati zahanati ya Ijumbi

Na Nyemo Malecela, Kagera

Katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora za afya, Serikali wilayani Muleba mkoani Kagera imetenga Sh milioni 60 kwa ajili ya kukarabati majengo matatu ya Zahanati ya Ijumbi yaliyotolewa kama msaada na mdau wa afya.

Majengo hayo matatu yaliyotolewa na mdau wa afya, Prosper Rweyendera ‘Mr PR‘ yalikabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dk. Leontine Rwamulaza amesema fedha hizo zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa zahanati hiyo ni Sh milioni 30 zilitokana na mapato ya ndani na Sh milioni 30 ni ruzuku kutoka serikali Kuu.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dk. Leontine Rwamulaza amesema fedha hizo zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa zahanati hiyo ni Sh milioni 30 zilitokana na mapato ya ndani na Sh milioni 30 ni ruzuku kutoka serikali Kuu.

Dr Rwamulaza alisema fedha hizo zimetengwa ni kwa ajili wa ukarabati wa majengo na miundombinu pekee wala hazihusishi vifaa tiba.

“Baada ya ukarabati huo kukamilika tutaanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje na mama na mtoto (OPD na RCH Clinic).”

Ili kuhakikisha zahanati hiyo inatoa huduma inavyotakiwa kwa wananchi wa kata ya Ijumbi na kata jirani, serikali pia imetenga shilingi milioni 45 kwa ajili ya kutengeneza barabara ya Ijumbi kupitia Kamwana Hadi Kamachumu.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA Wilaya ya Muleba, Mhandisi Dativa Teleciphone alisema barabara hiyo yenye urefu wa kilometa nne itajengwa kwa kiwango cha Changarawe.

“Utengenezaji wa barabara hiyo iliyoanza kujengwa kutoka Ijumbi kupitia Kamwana hadi Kamachumu itaambana na utengenezaji wa karavati tatu ambayo yamekuwa yakisababisha kupitika kwa shida.

“Ujenzi huu ulianza Aprili mwaka huu na unatarajia kukamilika Juni 27, mwaka huu kwa kuwa kwa sasa umefikia asilimia 50,” alieleza Mhandisi Dativa.

Naye Mr Pr amesema amejikuta akilazimika kuwekeza nyumbani alikozaliwa kwa sababu anapokuja likizo anashindwa kupata huduma za kijamii kwa urahisi.

“Mimi ni mzaliwa wa Ijumbi ila ninaishi kwenye mikoa mingine ambako ninapata huduma za kijamii za viwango vya juu lakini ninapolazimika kuja nyumbani na familia maisha yanakuwa magumu kutokana na kukosa huduma hizo.

“Lakini pia nina karibia kustaafu hivyo nitarudi nyumbani nilikozaliwa ndio maana nalazimika kuwekeza mapema,” amesema.

Mbali na kutoa majengo hayo tayari Mzee Pr amejenga kituo cha Polisi, nyumba za kuishi wa tumishi lakini pia ameshaanza kujenga majengo kwa ajili ya mahakama.

Naye Diwani wa Kata Ijumbi, Wilbad Kakuru alisema msaada wa ujenzi wa zahanati hiyo utasaidia kuhudumia wanakijiji 1,1000 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 wanaopatikana katika Kata hiyo yenye vijiji vitano na vitongoji 16 pamoja na kata jirani za Ibuga, Buangaza, Buganguzi na Kashasha.

“Wanakijiji wa kata zote hizo wamekuwa wakitegemea kupata huduma ya afya katika kituo cha afya cha Rubya kwa kuwa hakuna Kata kati ya hizo ambayo ina zahanati wala kituo cha afya.

Tumeupokea msaada huu kwa mikono miwili kwani tunategemea uwepo wa zahanati hii ya serikali utatupunguzia gharama za matibabu kwa kuwa zahanati tuliyokuwa tukiitegemea ni ya misheni hivyo inatoza gharama kubwa,” alisema.

Kakuru alimshukuru Mzee PR kwa msaada huo kwa kusema endapo wananchi wangetakiwa kuchangia gharama za ujenzi wa majengo ya zahanati hiyo ingewagharimu miaka 20 kukamilisha ujenzi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles