25.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 5, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI MOSHI YAWAONYA WAVAMIZI

Na UPENDO MOSHA, MOSHI


Kippi WariobaSERIKALI wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro, imewataka wananchi waliovamia  na kufanya shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwamo kilimo, ufugaji na kujenga nyumba za makazi katika maeneo ya  msitu wa kuzunguka  Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa), wahame.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba,  wakati akizungumza na viongozi wa Vijiji vya Uri na Omarini, vilivyopo Kata ya Kibosho Kati wilayani hapa.

Kippi alikuwa akizungumza na viongozi hao wakati wa uhakiki wa mipaka ya hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro na vijiji hivyo.

Alisema Serikali ya wilaya hiyo ina nia ya kuwaondoa wananchi wote waliovamia katika maeneo ya msitu wa kuzunguka hifadhi ya mlima huo wakati wowote kama hawataamua kuhama kwa hiari yao.

“Serikali imejipanga kuhakikisha tunawaondoa wananchi wote waliovamia katika maeneo haya na zoezi litaanza muda wowote kwani sheria zipo wazi na zinakataza mtu au watu kuvamia na kuendeleza maeneo ya hifadhi.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha maeneo yote yaliyohifadhiwa yanabaki kuwa salama kwa faida ya vizazi vijavyo na Serikali haipo tayari kuona maeneo hayo yanageuzwa kuwa makazi ya watu.

“Badala yake, tutahakikisha wale wote walioingia katika maeneo hayo wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

“Nasema hivyo kwa sababu kuna baadhi ya wananchi  kwa kushirikiana na  viongozi wa vijiji na vitogoji, wamevamia maeneo yaliyotengwa kisheria ili kuyalinda, lakini wao wamejaribu hata kubadili ramani za michoro ya vijiji na kuhamisha mawe ya mipaka kwa lengo la kuingilia hifadhi za Taifa.

 

Naye Mhifadhi Ujirani Mwema kutoka Kinapa, Hobokela Mwamjengwa, alisema uhakiki wa mipaka ulifanyika vizuri katika vijiji 65 ambavyo wameshavipitia.

Kwa upande wake, Ofisa Maliasili na Misitu, Mkoa wa Kilimanjaro, Emmanuel Kiyengi, alisema kila mwaka zaidi ya hekta 300,072 za misitu hapa nchini zinateketea kutokana na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na shughuli mbalimbali  za kibinadamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles