29.1 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUTENGA MAENEO MAALUMU YA VIJANA

|Bethsheba Wambura, Dar es Salaam



Serikali imesema iko kwenye mchakato wa kutenga maeneo maalumu ya vijana kufanyia shughuli zao za kijasiriamali ili kuwapa nafasi ya kujiajiri na kupunguza wimbi la vijana wengi kukaa mtaani bila ajira kutokana na kuzitaka manispaa zote nchini kutenga maeneo hayo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Anthony Mavunde, amesema hay oleo Agosti 29, jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua Maonesho ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph.

Amesema mpango huu unatekelezwa baada ya taarifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), kuonesha kuwa asilimia 70 ya vijana wanashinda vijiweni kutokana na kukosa ajira.

“Takwimu kutoka NBS baada ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonesha asilimia 70 ya vijana wanashinda vijiweni na kupiga stori na hii inatokana na wao kukosa ajira za kufanya na tunazitaka manispaa zote nchini kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya vijana kufanya shughuli zao za kimaendeleo,” amesema.

Aidha, amesema mipango mingine ya Serikali katika kutatua matatizo ya vijana ni kuyatambua makundi ya vijana, kutoa  elimu ya ajira na kuwarasimisha vijana wawe katika vikundi (Saccos na makampuni) ili mikopo inapotolewa iwafikie kwa urahisi.

Akizungumza wakati akimkaribisha Naibu Waziri, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Burton Mwamila amesema Uongozinwa chuo hicho umeamua kushirikiana na Wanafunzi ili kuyapata tija zaidi maonesho hayo baada ya wanafunzi kufanya kadhaa peke yao.

“Lakini pia, tumeamua kushirikiana na wanafunzi ili kuonesha watu kuwa chuo chetu kinatoa wahitimu waliowiva, wenye ubunifu wa hali ya juu na wana uwezo wa kujiajiri hivyo tunaiomba serikali iwape mazingira wezeshi ili mawazo yao yatumike katika kuendeleza sekta ya viwanda,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles