26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kukomesha uvuvi haramu Ziwa Victoria

Na Sheila Katikula,Mwanza

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema Serikali imejipanga kukomesha uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria.

Mvuvi wa Dagaa wa mwalo wa Rushanga kutokana wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Sospeter Ochieng akizungumza jana jijini Mwanza kwenye kikao cha wadau wa sekta ya uvuvi Kanda ya ziwa chenye lengo la kujadili changamoto za wavuvi.picha na Sheila Katikula.

Hayo ameyasema Mei 16, mwaka huu kwenye kikao cha Wadau wa Sekta ya Uvuvi Kanda ya Ziwa chenye lengo la kujadili changamoto za uvuvi kilichowakutanisha wavuvi, wachakataji wa mazao ya uvuvi,Watengenezaji na wasambazaji wa zana za uvuvi, wawakilishi wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba, wawakilishi wa usambazaji wa taa za sola, Watendaji wa Wizara.

Amesema kuendelea kwa uvuvi haramu kwenye ziwa Victoria kutasababisha kuwa janga ni vema kila mtu kulinda rasilimali za nchi kwa kufuata sheria kwa kuvua uvuvi halali.

“Mmekili uvuvi haramu umekithili mkiendelea kufanya hivyo samaki na dagaa wataisha na kutakuwa na janga kwani asilimia kubwa ya wananchi wanategemea ziwa victoria kwa kufanya uvuvi.

“Tunatakiwa tuulilinde ziwa letu ili tuendelee kufanya shughuli zetu za kujipatia kipato hivyo ni vema kila mtu anawajibu wa kubadilika kwanzia kichwani mpaka kwenye vitendo vyetu kwa kuvua uvuvi halali,” amesema Ndaki.

Amesema uvuvi haramu unaendelea hivi sasa unaanzia kwa mvuvi, msimamizi,viwandani Kwa sababu hawatoi taarifa pindi wanapoletewa samaki wadogo, kila mtu anawajibu wa kutoa taarifa ili kukomesha vitendo hivyo.

“Mtu wa kwanza anayeshiliki na uvuvi haramu ni mvuvi mwenyewe kwa sababu ndiye anakula kupitia hapo ni lazima kuwafichua wanaofanya vitendo hivi ili sheria ichukuliwe.

“Mkiendelea na uvuvi haramu tutatumia nguvu kukomesha vitendo hivi tusilaumiane maana tumepewa dhamana ya kulingana rasiliamali hizi ni lazima tuzilinde kwa hali na mali,” ameongeza Waziri Ndaki.

Nae, Mvuvi wa dagaa kutoka Mwalo wa Rushanga uliyopo Wilaya ya Muleba,
Sospeter Ochiengi ameiomba Serikali kuweka bei moja ya kulipia leseni ili waweze kulipa kwa wakati na kuepuka kukwepa.

“Sisi wavuvi wa Wilaya ya Mleba tunalipia bei kubwa ya leseni tofauti na wilaya nyingine kwani tunalipa Sh 170,000 kwa mtumbwi mpya lakini kwa mtumbwi wa zamani unalipia Sh 130,000 tunaomba leseni zinazotozwa zisitofautiane ili tupate unafuu wa kulipa bila kukwepa.

Hata hivyo, ameiomba Serikali kutowachulia hatua wamiliki wa mimbwi kwa makosa yanayofanywa na wavuvi na badala yake wawachukulie hatua wavuvi.

“Sheria inasema ukivua samaki wachanga unatakiwa uwarudishe ziwani na usiporudisha unachukuliwa hatua kali inaskitisha kuona tukosa la mvuvi linaletwa kwa mmiliki wa chombo ili alipe faini kulingana na kosa alilofanya mvuvi hii inaleta hasala kubwa kwani mwenye mali hausiki na hayo makosa na hajamtuma kufanya uharamia huo.

“Tunaomba makosa yatenganishwe kama ilivyo kwenye magari ili kila mtu abebe mzigo wake ili kuletwa usawa,” amesema Ochieng.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi wa samaki Mkoa wa Kagera, Medard Kaijage amesema kutokana na kukithili kwa uvuvi haramu wa kwenye ziwa Victoria kumepelekea samaki kukosekana ni vema serikali kuchuka hatua ili iwe fundisho Kwa watu wengine.

Ameiomba Serikali kuangalia upya sheria ya sola na kurudisha uvuvi wa karabai wa zamani ambao ulikuwa hauathili sanjari na kudhibiti utegaji wa samaki wa kutumia makokolo, timba na vyavu ambazo haziluhusiwi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles