25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TACAIDS yafanya kikao cha ufuatiliaji wa mwitikio wa UKIMWI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), imefanya kikao cha Kamati ya utekelezaji wa Programu ya Mwitikio wa UKIMWI nchini.

Kikao hicho kimefanyika leo Mei 17, 2022 jijini Dodoma kwa kushirikisha Menejimenti ya TACAIDS ambapo Mwendeshaji wa kikao hicho ni Kamisheni ya Tume hiyo.

Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya utekelezaji wa Program za Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS) wakifuatilia mada mbalimbali za kikao hicho kilichofanyika Mei 17, 2022 jijini Dodoma.

Lengo la Kikao hicho ilikuwa ni kufanya ufuatiliaji wa shughuli zinazotekelezwa na TACAIDS kuona kama zimetekelezwa kwa malengo yaliyokusudiwa kwenye Sheria ya Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania Na. 22 ya mwaka 2001 na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 2015 na kuwafikia walengwa kama ilivyotarajiwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Programu, Sheikh Khamis Mataka, amesema vikao hivyo ni moja ya ufatiliaji wao kama viongozi wa Tume kufahamu kwa kina namna shughuli zinavyotekelezeka kuendana na mipango iliyopangwa na Tume.

“Vikao hivi kwetu ni muhimu sana kwani huwa tunashiriki wakati wa upangaji kabla bajeti haijapelekwa Bungeni na baada ya kurejea huwa kuna utekelezaji ambao hufanywa na wataalamu wetu, kabla ya kukaa kikao kikubwa cha kamisheni tunakaa kwanza na wataalamu wanatupatia utekelezaji wa mipango yao na kuona kama imeendana na makubaliano tuliyoyaweka awali,”alisema Sheikh Mataka.

Mwenyekiti wa Kamati ya Utekelezaji wa Program za Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS), Sheikh Khamis Mataka (kushoto) akifungua kikao hicho kinachofanyika leo Mei 17, 2022 jijini Dodoma, kulia ni Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi kutoka TACAIDS, Jumanne Isango.

Kikao hiki ni utangulizi wa vikao viwili vya programu vilivyopangwa kufanyika wiki hii kwa lengo la ufuatiliaji wa utekelezaji wa majukumu ya TACAIDS kulingana na utaratibu uliowekwa na Kamisheni ya Tume ambayo imeundwa kwa mujibu wa sheria iliyounda TACAIDS.

Nae, Mratibu wa vikao hivi ambaye pia ni Mwanasheria wa TACAIDS, Miraji Mambo amesema kamisheni ya TACAIDS imeundwa kwa mujibu wa sheria na ina wajumbe kumi na moja, ambao ndio wanaongoza TACAIDS kwa kusimamia sekretarieti katika utekelezaji wa majukumu yote ya Tume.

Mambo amesema kuwa kwa mujibu wa utaratibu kamati hizi zipo mbili; Kamati ya programu, ilikutana leo Mei 17, 2022, ambayo inafuatilia zaidi utendaji wa shughuli za tume na kamati nyingine ya fedha itakutana Mei 18,2022 ambayo kazi yake kubwa ni kuangalia kwa kina matumizi sahihi ya fedha za TACAIDS.

Aidha, kikao cha 49 cha Kamisheni hiyo kinatarajiwa kufanyika Mei 24, 2022 kwa ajili ya kujadili pamoja na mambo mengine taarifa kutoka kwenye Kamati ya Utekelezaji wa Programu na Kamati ya Fedha.

Baada ya kumaliza kikao mwenyekiti ameishukuru Sekretarieti kwa maandalizi mazuri ya taarifa za utekelezaji wa programu na kuagiza utaratibu huo waendelee nao kwa maana kwamba Kamisheni ifanye kazi yake na sekretarieti ifanye kazi yake ili kufikia malengo ya Tume yaliyosukudiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles