25.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuchukua uamuzi mgumu mwendokasi

Na GRACE SHITUNDU-DAR ES SALAAM

SERIKALI imeahidi kuchukua uamuzi mgumu ndani ya siku tatu i kutatua changamoto kuhusu uendeshaji wa mradi wa Mabasi ya Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart).

Ahadi hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kutembelea kituo cha Kimara.

Alisema kutokana na hali hiyo atasimamia upatikaji wa mabasi 20 kwa ajili ya kusaidia kusafirisha wanafunzi.

Makonda alitoa uamuzi huo    siku moja baada ya abiri  wanaotumia usafiri huo kushindwa kuvumilia na  kuingia barabarani kwa kukosa usafiri wa uhakika kuwahi kwenye shughuli zao.

Makonda pamoja na watendaji wa serikali wakiwamo wa Wakala wa Usafiri wa Mabasi ya Haraka Dar es Salaam (Dart) alifika Kimara saa 12:30 asubuhi na kuzungumza na wananchi.

Aliwaomba radhi kutokana na kero wanazokumbana nazo kwenye usafiri huo.

“Ninakwenda kuonana na Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo ili yeye aje atoe tamko mabasi yanaongezwa lini, utaratibu wa nauli unafanyikaje, lini wananchi watakuwa wanalipa kwa kadi, waache usumbufu kuwa wanakata tiketi kila siku ili kuokoa fedha  lakini pia kuokoa matapeli wanaojipatia fedha  kwa njia za panya.

“Pia hakuna dereva kupaki gari, kama umekuja asubuhi kwa ajili ya kuendesha na ukapaki ni kinyume cha sheria.

“Tutakukamata na kukufungulia mashtaka kwa kuwa utakuwa umevunja sheria na mkataba wako wa kazi,” alisema Makonda.

Alisema kutokana na msongamano, kuna hatari kubwa ya watu kuambukizana magonjwa hasa ya Kifua Kikuu (TB).

“Wewe fikiria kama kuna mtu ana ugonjwa wa Kifua Kikuu, kwa hali ilivyo hapa maana ni rahisi watu wengi kuambukizwa.

“Rais hakuwekeza kwenye mwendokasi   watu wagombanie, aliwekeza mwendokasi   watu wawahi  kazini tena wakiwa wasafi na wastaaarabu,” alisemas Makonda.

Makonda alisema kwa sasa watu wamekuwa wakikumbana na changamoto lukuki kwenye usafiri huo ikiwamo kutoka nyumbani wakiwa wasafi lakini wanapofika kazini nguo zao hujikuta zimeharibika kwa kugombania magari.

Alisema hali hiyo imechangia pia wezi kutumia mwanya huo kuwaibia abiria wanaotumia usafiri huo simu, pochi na hata fedha.

“Kwa hiyo niwatake walinzi wanaohusika katika vituo vya mabasi haya  kuhakikisha kwamba hakuna wizi unaotokea.

“Rais (Dk. John Magufuli),  aliagiza kufungwe kamera, hivyo zitumike pia kulinda mali za raia,” alisema

Aliwataka wahudumu wa kukatisha tiketi na askari wa ulinzi katika vituo hivyo kuwahudumia watu na kuacha tabia ya kuwanyanyasa wananchi.

Makonda  alitoa wito kwa abiria kuwapiga picha na kuwarekodi wahudumu wanaowanyanyasa wananchi na kuzisambaza kwenye mitandao ya jamii waovu waweze kuonekana kwa haraka.

“Niwaombe wananchi mtakapoona mtu yoyote aliyeko kwenye kituo cha mwendokasi awe dereva, mkatisha tiketi au askari, wewe akikunyanyasa, cha kufanya mrekodi tu kwa simu yako na ukisambaza kwenye mitandao tutaiona,” alisema.

Aliwaambia wananchi kwamba wana haki ya kupiga picha kituo chochote cha mwendokasi na hawazuiwi na mtu yeyote.

Kuhusu wanafunzi, Makonda alisema ofisi ya mkoa ina mpango wa kuingiza mabasi 20 maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa mkoa  huo.

Katika hatua nyingine Makonda aliamuru wafanyabiashara wa Kimara kutumia eneo la Tanroads wakati wanasubiri kutafutiwa eneo jingine la kudumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles