25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Serena, venus umri sio tatizo kwenye tenesi

Serena Williams
Serena Williams

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO,

Michuano ya tenisi imefikia mwisho wiki iliopita tukiwaona nyota bora duniani kwa upande wa wanawake, Serena Williams na dada yake Venus Williams wakitamba kwenye michuano hiyo.

Kulikuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na wanawake wengi kuonesha uwezo wao kwenye michuano hiyo hasa kutokana na umri wao.

Hata hivyo hali hiyo ya ushindani haikuwapa shida wakongwe hao kwenye tenisi ambao wanaonekana kuwa na umri mkubwa na bado wakionesha kiwangu kikubwa.

Kutokana na umri wa Venus na Serena, wengi waliamini kwamba wababe hao hawawezi kufika mbali kutokana na vijana wa sasa kufanya vizuri zaidi.

Katika michuano ya Wimbledon ambayo imemalizika mwishoni mwa wiki iliopita, Serena alifanikiwa kufika hatua ya fainali huku dada yake Venus akiishia hatua ya nusu fainali.

Baada ya wawili hao kufikia hatua ya nusu fainali wengi walianza kuamini kwamba watoto hao wa mzee Williams watafika wote fainali hivyo taji hilo la Wimbledon litakwenda kwao.

Hata hivyo hali ilikuwa tofauti kwa Venus mwenye umri wa miaka 36, ambaye aliwahi kuwa bingwa namba moja kwa ubora duniani na sasa anashika namba 9, yeye hakuweza kusonga hatua ya fainali kwa kuwa alitolewa na mpinzani wake Angelique Kerber, raia wa nchini Ujerumani mwenye umri wa miaka 28, huku akiwa anashika nafasi ya 92 kwa ubora duniani.

Kwenye mchezo huo Angelique alionesha uwezo wake na kufanikiwa kuingia hatua fainali kwa seti 6-4, 6-4 na kumfanya akutane na bingwa namba moja kwa ubora wa mchezo huo Serena.

Hii ilionesha wazi kwamba umri wa Serena na Venus bado sio tatizo kwenye mchezo huo, kwa kuwa wao walionekana kuwa na umri mkubwa kuliko washiriki wengine, lakini mmoja ambaye ni Venus alifikia hatua ya nusu fainali huku Serena mwenye umri wa miaka 34, akifika fainali.

Serena alitumia dakika 48 kufanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kumchapa mpinzani wake Elena Vesnina ambaye anashika nafasi ya 21 kwa ubora duniani, huku Serena akishinda kwa seti 6-2, 6-0.

Venus Williams
Venus Williams

Hata hivyo Serena alitamani kukutana na dada yake katika mchezo wa fainali kwenye michuano hiyo ya Wimbledon huku akiamini kwamba mmoja wao ataweza kuchukua taji hilo na kupeleka heshima kwenye familia ya Williams.

Serena amekuwa na rekodi bora kwenye michuano mikubwa ya Grand Slam, ambapo amefanikikiwa kuchukua taji la wazi la Australia mara sita, French Open mara tatu, Wimbledon mara sita pamoja na michuano ya wazi ya US mara sita.

Wakati huo dada yake Venus, amekuwa na rekodi kubwa kama vile kutwaa taji la Wimbledon mara tano, US Open mara mbili huku mwaka 2003 akishindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Australia Open na 2002 kwenye michuano ya French Open.

Katika fainali hizo za Wimbledon kwa upande wa wanaume, Andy Murray ambaye anashika nafasi ya pili kwa ubora duniani kwenye tenisi, alifanikiwa kufika fainali baada ya kumchapa mpinzani wake Tomas Berdych raia wa Jamhuri ya Czech na kumfanya fainali acheze na Milos Raonic raia wa Cadana mwenye umri wa miaka 25.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles