27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Selena Gomez: Nipo ‘single’ kwa sasa

Selena Gomez's new Spring/Summer fashion collection for adidas NEO LabelNEW YORK, MAREKANI

MSANII wa muziki na filamu nchini Marekani, Selena Gomez, amedai kuwa yeye ni msanii pekee anayeishi bila mpenzi kwa sasa.

Msanii huyo amejitofautisha na nyota wengine wanaofanya vizuri kama vile Taylor Swift na Gigi Hadid.

Mrembo huyo amedai tangu aachane na nyota wa muziki raia wa Canada, Justin Bieber, amekuwa hakai na mwanaume kwa muda mrefu.

“Hakuna kisichowezekana, awali nilidhani siwezi kuachana na Justin Beiber, lakini niliweza kuachana, nikawa najiuliza nitaishi vipi bila yeye ila inawezekana na sasa naishi bila mwanaume.

“Nadhani nipo peke yangu kwa sasa kwa wasichana maarufu ambao wanaishi bila wapenzi, najua Taylor Swift, Gigi, Kendall Jenner na wengine wengi wana wapenzi, hivyo wamekuwa tofauti na mimi,” aliandika Selena kwenye akaunti yake ya Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles