25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Sekondari ya Eagles yazindua mfumo wa kielektroniki kufuatilia maendeleo ya wanafunzi

Mwandishi Wetu, Bagamoyo



Shule ya Sekondari ya Eagles ya Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani, imefanya sherehe za mahafali yake ya 10 na kuzindua rasmi mfumo mpya wa Menejimenti ya Shule ambao utasaidia wazazi kufuatilia maendeleao ya watoto wao kwa ukaribu zaidi.

Akizundua mfumo huo sanjari na kutoa neno kwa wahitimu 71 wa kidato cha nne wa shule hiyo,  mgeni rasmi Mkaguzi na Mdhibiti wa Elimu Bora Wilaya ya Bagamoyo, Davis Moye amewataka kuzingatia maadili na kujiandaa vyema kwa mitihani yao hiyo ya kuhitimu.

“Mjiandae vyema na mtafanya vizuri kwenye mitihani yenu, lakini pia nitumie nafasi hii kuwapongeza uongozi wa Eagles kuja na mfumo huu ambao utasaidia wanafunzi na walimu kufanya mambo kiufanisi zaidi,” amesema Moye.

Hata hivyo, amewataka wazazi kufuatilia na kuwa karibu na watoto wao ili kubaini mapungufu kwa hatua ya kuyatatua.

Naye Mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo, Eva Fumbuka amejivunia kufanya vizuri kitaaluma na kuongeza kuwa lengo la shule hiyo ni kuwa shule bora kitaifa.

“Eagles mwaka 2006, ilikuwa ya kwanza kwa wavulana kwa Wilaya ya Bagamoyo, leo katika mahafali ya 10, matamanio yetu ni kufikia nafasi za juu zaidi kitaifa.

“Tumefanikiwa kutunukiwa vyeti vya shule bora kwa muda wa miaka mitatu mfululizo na kwa kipindi cha miaka tano, pia ni mara ya tatu kupata mwanafunzi bora kwenye 10 bora kitaifa” amesema Mwenyekiti huyo wa Bodi.

Kwa upande wake Meneja wa shule hiyo, George Fumbuka amewashukuru wazazi kwa kuwaamini na hivyo wataendelea kufanyia kazi mapungufu  huku  wakitarajia kuanzisha kozi zaidi shuleni hapo ili kuendana na matakwa ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles