24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

SCORPION JELA MIAKA SABA

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemtia hatiani Salum Njwete maarufu Scorpion kwa kosa moja la kumjeruhi mfanyabishara Saud Mrisho na kumhukumu kifungo cha miaka saba jela.

Scorpion amehukumiwa leo Jumatatu, Januari 22 katika Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Flora Haule.

Mahakama pia imemuachia huru kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha kwa sababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kosa hilo bila kuacha shaka.

Pamoja na kwenda jela miaka saba, mahakama imeamuru alipe faini ya Sh milioni 30 kama fidia kwa mlalamikaji.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Scorpion inadaiwa aliiba mkufu wa rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 ukiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili ya mkononi na fedha taslimu Sh 331,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh 476,000, mali ya Said Mrisho.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kabla na baada ya wizi huo, alimchoma kisu tumboni, mabegani na machoni mlalamikaji huyo ili aweze kujipatia mali hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles