23.6 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Sartimes yawatajirisha wasanii wa filamu nchini

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Filamu zaidi ya 120 za Wasanii wa Tanzania zimenunuliwa na chaneli mpya ya St Swahili Plus chini ya Startimes Media kwa ajili ya kuoneshwa kwa watazamaji.

Akizungumza Mei 20, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati uzinduzi wa chanel hiyo,
Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa Startimes, David Malisa amesema hiyo yote ni kuunga mkono juhudi za wasanii katika kazi zao lakini pia, kuhakikisha wanatoa burudani kwa Watanzania.

“Tumeanzisha chanel ambayo silimia 60 ya maudhui yanatoka ndani ya nchi. Tumetoa fursa kwa wasanii kwa kununua kazi zao ili na wao waweze kunufaika lakini pia na watazamaji wetu waburudike, jambo la muhimu tumekuja na kampeni ya kamatia furushi watu walipie vifurushi kuanzia Sh 23,000 wanufaike,”amesema.

Malisa amesema uzinduzi huo umeenda sambamba maudhui mengine ya chaneli nyingine mpya kama ST Toons, ST Toonie, ST Kids Plus, ST movies kwa ajili ya kuonesha vipindi mbalimbali vya tamthili, watoto nafilamu.

Mwakilishi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Edward Nnko amewapongeza Startimes kwa kutoa fursa kwa Watanzania akisema imekuwa ikitoa nafasi ya watu mbalimbali duniani kujifunza Kiswahili kupitia vipindi tofauti.

“Nawahimiza Watanzania waendelee kukamatia fursa unaweza kusema sio Kamatia furushi tu, bali kamati fursa, elimu ya kujifunza, kuburudika na kwa uhakika watajisikia furaha,” amesema.

Mwakilishi wa wasanii Rashid Mrutu amesema tangu 2018 wamekuwa wakikusanya Maudhui mbalimbali ya filamu na wamehusika kukusanya filamu nyingi za Kitanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles