29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Saratani yazidi kuwa tishio kwa wanawake

Dk. Julius Mwaiselage
Dk. Julius Mwaiselage

NA HADIA KHAMIS, DAR ES SALAAM

UNGONJWA wa saratani umezidi kuwa tishio nchini hususan kwa wanawake, kwani idadi ya wagonjwa inaongezeka kwa asilimia 100.

Akizungumza katika Madhimisho ya Siku ya Mandela jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage, alisema  wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 45 wanaongoza kwa saratani ya shingo ya kizazi kwa asilimia 40.

Alisema  utafiti uliofanywa tangu mwaka 2,000 hadi 2016 umebaini idadi ya wagonjwa wa saratani inazidi kuongezeka hadi kufikia wagonjwa 5,700.

“Tatizo la saratani ni kubwa tofauti na watu wanavyolichukulia, katika taasisi yetu hadi sasa tuna wagonjwa 300 wakiwamo wanawake 200 na wanaume 100, lakini wagonjwa waliopo nje ya taasisi ni wengi sana,”alisema Dk.Mwaiselage.

Alisema matibabu ya saratani yanachukua miaka 15 hadi 20 hadi kupona kabisa.

“Matibabu ya saratani yanachukua muda mrefu ni vema wananchi kufanya vipimo mapema ili kufahamu kama wamepata maambukizi au laa, pia itasaidia kupata matibabu mapema,”alisema.

Hata hivyo, alisema taasisi ya Ocean Road inakabiliwa na changamoto kubwa ya gari ya wagonjwa, kwani hadi sasa wana gari moja ambalo hurudisha nyuma utoaji wa huduma kwa wagonjwa kwa wakati.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini Tanzania, Dk. Rufaro Chataora, alisema kwa kuheshimu mchango mkubwa uliotolewa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ni wajibu wa kila mtu kuwajali na kuwasaidia wagonjwa wa kansa.

Alisema Mandela alitumia dakika 67 katika kuhakikisha watu wa Afrika Kusini wanapata uhuru wao, wakiwamo wafungwa na walemavu kuwa na maisha bora na kuhakikisha matibabu bure kama ilivyo kwa taasisi hiyo.

Alisema ugonjwa wa kansa unatibika hivyo ni vema watu wakajenga tabia ya  kufanya mazoezi ili kujiepusha na maradhi hayo.

Hata hivyo, Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleka, alisema Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya Nelson Mandela kwa kutambua mchango wake katika jamii.

Katika maadhimisho hayo, Afrika Kusini ilitoa msaada wa chakula kwa wagonjwa waliolazwa katika taasisi ya Ocean Road, huku akisisitiza kuwa wagonjwa wa saratani wana haki ya kupendwa na kuheshimiwa kama wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles