23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

Yanga: Hatupo tayari kumwachia Pluijm

pluijm na manji

NA ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema kuwa haupo tayari kumwachia kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van Pluijm, huku ukieleza kwamba kwa sasa upo mbioni kumwongezea mkataba mpya ili kuendelea kukinoa kikosi chao kwa mafanikio msimu ujao.

Kauli hiyo ya Yanga imekuja siku chache baada ya kocha huyo kutwaa tuzo ya Kocha Bora katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, pia kuisaidia timu hiyo kuwa bingwa wa ligi hiyo mara mbili mfululizo tangu msimu wa 2014/15 na 2015/16 pamoja na kushiriki hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza na MTANZANIA jana Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Baraka Deusdedit, alisema kwamba kutokana na mafanikio waliyoyapata tangu Pluijm atue kwenye klabu hiyo si rahisi kumtimua kwa kipindi hiki.

“Tunaendelea kujadili namna ya kuongeza mkataba wa Pluijm, huenda siku chache kutoka sasa tukampa mkataba huo kwani bado tunamhitaji kwa kuwa tuna matumaini naye.

“Michezo mitatu aliyopoteza katika michuano ya Kombe la Shirikisho haitoshi kumfukuza, tunataka kumpima kwa kumpa muda mwingine zaidi wa kukinoa kikosi chetu,” alisema Deusdedit.

Katibu huyo aliongeza kuwa klabu hiyo kwa sasa inajipanga kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika michezo iliyopita ya kimataifa na kitaifa ili kufanya vizuri zaidi msimu ujao.

“Lengo letu kimataifa ni zaidi ya tulipofikia sasa, hivyo ni jukumu letu kushirikiana na kocha ili tufike tunapopataka,” alisema Deusdedit.

Hata hivyo, katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ina pointi moja huku kinara, TP Mazembe ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Mo Bejaia yenye pointi tano na Medeama yenye pointi mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles