23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SANAA NI KIWANDA IPEWE NAFASI YA KUKUA

TANZANIA ya viwanda ndiyo ndoto inayootwa na Watanzania wengi wapenda maendeleo, ikiwa imeasisiwa na Rais Dk. John Magufuli. Na lengo kuu la wazo hilo la viwanda ni kuzalisha ajira kwa vijana.

Kama ni hivyo basi sekta ya sanaa ni kiwanda hai ambacho kimeendelea kuzalisha ajira lukuki kutokana na ukuaji wake wa kasi unaozihusisha sekta nyingine.

Hapa nitazungumzia sanaa ya muziki pekee kwa kuwa ndiyo imeonekana ikikua zaidi ya nyingine. Haina ubishi kuwa matamasha yamekuwa kiungo kikuu cha kukuza kiwanda hiki.

Mbali na burudani inayotolewa na wasanii juu ya jukwaa, watu mbalimbali huuza bidhaa zao kama vyakula nk kipindi chote yanapofanyika matamasha hayo.

Tunaona hayo linapofanyika tamasha la Sauti za Busara kule Zanzibar. Wajasiriamali wengi hujipatia fedha kutokana na ukubwa wa tamasha hilo linalowakutanisha wateja na wachuuzi wa bidhaa mbalimbali.

Kwa hiyo utaona sanaa ya muziki pekee imesababisha ajira kwa wajasiriamali wengine wengi. Hata kipindi cha tamasha na tuzo za nchi za Jahazi (ZIFF) huko huko Zanzibar.

Haina ubishi kuwa vijana wa Kizanzibari wanatengeneza fedha kwa zile siku zote za tamasha na tuzo za ZIFF, hivyo haina ubishi kuwa sekta ya sanaa ni kiwanda hai ambacho kinapaswa kupewa nafasi ili kikue zaidi.

Lakini pia leo linafanyika tamasha kubwa la Fiesta hapa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Leaders, tamasha hilo ambalo limetengeneza ajira nyingi toka siku ya kwanza lilipoanza kufanyika jijini Arusha.

Nyuma ya burudani itakayotolewa na wasanii kwenye jukwaa, kuna biashara nyingi kubwa na ndogo ndogo zinafanywa na wajasiriamali. Lakini jambo ambalo limeonekana kulaaniwa na wadau wengi wa burudani ni kufupishwa muda wa tamasha hilo uliopelekea kupunguzwa wasanii zaidi ya 20.

Nyuma ya wasanii hao walioikosa Fiesta mwaka huu kuna vijana wengi wamekosa ajira, maana msanii mmoja anakuwa na watu wasiopungua wanne nyuma yake.

Msanii mmoja anatoa ajira kwa mpiga picha, dansa wa 4 na ‘make up artist’, hivyo asipopata ajira ya kutumbuiza na hao watu nyuma yake wanakosa ajira. Ushauri ni vyema sekta ya sanaa ikapewa uhuru ili ikue na si kudumazwa kwa namna yoyote ile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles