23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Samatta, Ulimwengu watupwa kwa Waarabu CAF

Samatta-UlimwenguNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

BAADA ya timu ya TP Mazembe (DRC) wanayochezea Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa itakuwa na shughuli pevu kufika fainali baada ya kupangiwa Waarabu.

Samatta ndiye aliyekuwa chachu ya Mazembe kufika hatua hiyo baada ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’, wakati miamba hiyo ilipoifunga Moghreb Tetouan ya Morocco mabao 5-0 wikiendi iliyopita.

Mabao hayo yalimfanya Samatta kuondoa ukame wa kufunga mabao kwenye mechi saba zilizopita, mara ya mwisho kufunga kwenye michuano hiyo ilikuwa ni miezi mitano iliyopita walipoifunga Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) 3-1 Aprili 5.

Mazembe sasa ina mtihani mwingine mgumu zaidi ili kutwaa kombe hilo, kwani imepangwa kucheza na timu za Kiarabu, El Merreikh ya Sudan kwenye nusu fainali na ikiitoa italazimika kupambana na mshindi wa nusu fainali nyingine kati ya Wasudan wengine, Al Hilal na U.S.M Alger ya Algeria.

Akizungumza na MTANZANIA kutoka nchini humo jana, Samatta alikiri ugumu kwenye mchezo huo kutokana na kocha wa El Merreikh, Diego Garzitto, kuwahi kuinoa Mazembe kwa mafanikio mwaka 2003-2004 na 2009-2010.

“Kuna sababu mbili au tatu za ugumu, kwanza kocha wao anatufahamu. Pia tumeshawahi kukutana nao mara kadhaa. Pia kuna upinzani wa kimpira kati ya klabu za Kongo na Sudan kwa miaka ya hivi karibuni,” alisema.

Samatta pia aliizungumzia ‘hat trick’ yake ya hivi karibuni na kusema kuwa: “Najisikia furaha kwanza mimi binafsi kwa kuwa mmoja wa wachezaji walioweka rekodi ya kufunga hat trick, pia kwa kuiwezesha timu yangu kuingia kwa kishindo nusu fainali.”

TP Mazembe kwa sasa imepania nasaka kurudia rekodi ya mwaka 2010, walipotwaa ubingwa wa Afrika na kufika fainali ya Kombe la Dunia la klabu na kufungwa na Inter Milan ya Italia mabao 3-0.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles