22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Samatta kuweka historia Wembley leo

LONDON, ENGLAND

NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta, ambaye anakipiga katika klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu nchini England, leo atakuwa kwenye Uwanja wa Wembley kukipiga dhidi ya Manchester City.

Samatta ataongoza safu ya ushambuliaji ya Aston Villa kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu nchini England.

Hii ni mara ya kwanza kwa mchezaji wa kitanzania kucheza michuano hiyo ya Carabao pamoja na kucheza fainali kwenye uwanja huo wenye historia kubwa nchini England.

Samatta alijiunga na Aston Villa wakati wa uhamisho wa dirisha dogo la usajili la Januari mwaka huu akitokea katika klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu kwa kipindi cha misimu minne.

Hadi sasa tangu asajiliwe, amefanikiwa kucheza jumla ya michezo mitatu ya Ligi Kuu nchini Uingereza na kufanikiwa kupachika bao moja kwenye mchezo dhidi ya Bournemouth, huku Aston Villa wakipigwa mabao 2-1.

Samatta amedai kucheza kwenye Uwanja wa Wembley dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England kwake ni kama ndoto, hivyo lazima apambane ili kuiandikia historia klabu yake na yeye mwenyewe kwa ujumla.

“Haya ni mafanikio makubwa kwangu kwenda kucheza fainali ya Kombe la Carabao kwenye Uwanja wa Wembley dhidi ya Manchester City moja kati ya klabu kubwa duniani. “Sijawahi kucheza kwenye uwanja huo hapo awali, hii ni nafasi ya kipekee kwenda kuonesha uwezo wangu, ninashukuru kwa sasa nimezoeana na kila mchezaji ndani na nje ya uwanja, hivyo kilichobaki ni kuhakikisha tunalipigania taji hilo, kwa pamoja tunaamini tunaweza kuishangaza dunia japokuwa wapinzani wanatajwa kuwa bora zaidi, ila soka ni

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles