26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

SALMA HAYEK ASAIDIA WAHANGA WA TETEMEKO MEXICO

MAYAN, MEXICO

NYOTA wa filamu na mitindo nchini Marekani, Salma Hayek, ameshindwa kuzuia hisia zake kwa wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Mexico na kudai kuwa yupo tayari kuchangia kiasi cha dola 100,000, zaidi ya Sh milioni 222 za Kitanzania.

Msanii huyo ambaye alizaliwa mjini Coatzacoalcos nchini Mexico mwaka 1966, amedai kuguswa na tukio hilo ambalo limepoteza maisha ya watu zaidi ya 60.

Msanii huyo jana alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuwaomba watu wengine waungane na yeye ili kuweza kuwasaidia wale waliokumbwa na tetemeko hilo.

“Watu wa nchini kwangu Mexico wamekumbwa na majanga matatu sasa, watoto wengi wapo kwenye wakati mgumu na watu wengi wamekosa makazi. Kwa upande wangu nipo tayari kuchangia dola 100,000 kwa Unicef ili waweze kuwafikishia wahanga, tafadhali naomba ungana na mimi na uchangie ulichonacho, asanteni sana,” alisema Salma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles