MWANDISHI WETU
SUALA la usafi ni jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa na kila mwanajamii. Usafi wa mazingira usipozingatiwa ipasavyo huwa ni chanzo cha maradhi ya mlipuko na mengine mengi.
Inashuhudiwa kuwa watu waishio katika mazingira machafu ndio wanaoongoza kwa kukabiliwa na maradhi ya kila aina ikiwamo ya ngozi na hata kuhara.
Lakini, suala ambalo ni la msingi na linalopuuzwa na watu wengi ni usafi wa bafu (sehemu inayotumika kuogea). Watu wengi wamekuwa hawazingatii usafi wa mara kwa mara wa bafuni na badala yake hujikita zaidi vyooni (kunakotumika kujisaidia) aidha ni kwa sababu ni eneo ambalo halionekani ni hadi mtu aingine kuoga au ni uvivu tu wa watu waishio eneo husika.
Wiki kadhaa zilizopita, watatifi nchini Uingereza walifanya utafiti kuhusu usafi wa bafuni na umuhimu wake.
Watafiti hao wanasema usafi wa bafuni ni jambo linalopaswa kuzingatiwa zaidi kuliko watu wanavyodhani. Lakini inaonekana kuwa usafi wa bafuni umekuwa ni mgumu mno, kama ambavyo Profesa John Oxford, wa Chuo Kikuu cha Queen Mary University cha London, anavyosema: “Bafu ni mahali ambapo usafi wake huwa ni mgumu mno. Watu hutumia muda mwingi kusafisha vyoo vyao, lakini ingelikuwa vyema kama kila mtu angezingatia zaidi usafi wa bafu kwa kutumia dawa za kuuwa bakteria.”
Bomba la mvua/shower
Kuna baadhi ya familia huwa hawaogi kwa kutumia ndoo na kopo, yaani kujimwagia maji wenyewe, badala yake huoga kwa kutumia kifaa cha kumwagia maji mwilini kwenye bafu za manyunyu.
Wataalamu wanasema unapotumia kifaa hiki kwenye bafu za manyunyu hunabudi kuwa makini, kwani kinapotumika baada ya kuzimwa kwa muda mrefu na kutumiwa tena hugeuka kuwa makao ya vimelea vya bakteria.
Kwa kawaida bomba la mvua (shower) hutoa maji ya aina mbili, ya moto na ya baridi. Hatari inayoweza kuwakabili watu wazima na watoto itokanayo na kifaa hicho ni uwezekano wa kuunguzwa na maji yanayotoka kama mtu anahitaji kuoga maji ya moto, ambayo yanaweza kuwa moto zaidi na kuuchoma mwili.
Akizungumza na BBC, Msemaji wa kituo cha utafiti Rospa anasema: “Tunawaomba watu kuweka maji baridi kwanza ndani ya beseni/vidimbwi vya maji ya kuoga kwa ajili ya watoto. Kwa kufanya hivyo unawaepusha na hatari ya kuungua wanapojaribu kujifungulia maji ya moto.
“Kuna uwezekano mkubwa kwamba pale unapoweka maji moto kwenye beseni/ama kidimbwi cha maji ya kuoga watoto wanaweza kuyanawa na kuungua, lakini unapoweka maji ya baridi kwanza ndani ya beseni na baadae kuyachanganya na Ruksa kisheria kumuacha mwenza aliye gerezani muda mrefu ya moto, uwezekano watoto kuungua unakuwa ni mdogo.”
Sabuni ya kuogea Kwa kawaida unapotumia kipande cha sabuni kwa ajili ya kuoga, unatarajia kitasafisha mikono yako kwa hivyo, si rahisi kufikiria kwamba kinaweza kuwa kitovu cha vimelea vya maambukizi.
Profesa wa Oxford anasema: “Bakteria wanaweza kukaa kwenye sabuni ya kuogea na kuhama kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine – mfano bakteria aina ya E.coli ambao huishi maeneo ya bafuni.
“Ikiwa mtu atatoka nje ya kikundi cha familia akiwa na bakteria ama mmoja wa familia akipata bakteria hao, basi ni rahisi kuwaacha bafuni na kusababisha bakteria
kuzaliana na kuishi humo hatimaye kusambaa kwa familia nzima.”
Profesa huyo anashauri matumizi ya sabuni ya maji zaidi kuliko kipande cha sabuni kwa matumizi ya kifamilia.
Hii ni kwa sababu bacteria huwa si rahisi kukaa kwenye sabuni ya maji.
Taasisi ya kitaifa ya afya na ushauri bora wa kiafya nchini Uingereza, iliwashauri maafisa wa afya nchini humo kutumia sabuni za maji ama zilizowekwa kwenye
chupa kwa ajili ya kunawa mikono.
Taulo pia si salama Wataalamu hao wanasema taulo salama ni ile ambayo imekaushwa vizuri na pengine ikaipigwa pasi. Wanasisitiza ni bora zaidi kukausha mikono ama uso kwa kutumia taulo hilo unapokuwa na maji nyakati za mchana.
“Lakini usiruhusu kwa namna yoyote ile mtu mwingine alitumie taulo lako kwani ni
kitu chenye utata,” anasema Profesa Oxford na kuongeza: “Usithubutu hata siku moja
kutumia taulo moja na mtu mwingine – sishauri hilo.”
Huwa ni jambo la kawaida kwa watu kutumia taulo moja katika maeneo ya sinki za bafuni/chooni ambayo hutumiwa na wanafamilia na hata marafiki wanaotembelea sehemu husika.
Hata hivyo, Profesa Oxford anasema:
“Ni heri kuepukika hilo. Vimelea vya magonjwa/ bakteria vinaweza kukaa kwenye taulo kwa saa nne. Kusema ukweli taulo ni mahala pazuri kwao kukaa kwa sababu hewa imefunikwa na kuwa nzito
“Ningeshauri karatasi laini zitumike kukausha mikono badala ya taulo na kutupwa kwenye debe la taka au kila mtu awe na taulo lake.”
Ni hatari kuwaogesha watoto wakiwa na mdoli wa plastiki bafuni Utafiti umebaini kuwa kumuacha mtoto kuingia bafuni akiwa na mdoli au kifaa kingine kunaweza kusababisha hatari kubwa kiafya.
Gazeti la Times liliripoti juu ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Uswiss ya Sayansi na Teknolojia, ambapo watafiti walifanyia uchunguzi midoli inayochezewa na watoto wakati wa kuoga na kubaini kuwa asilimia 58 ya midoli hiyo ilikuwa na bakteria hatari aina ya fangasi.
Mkuu wa utafiti huo anaonya watu wasiwarushie watoto wao maji usoni kwa kutumia mdoli wa kuchezea kwa sababu unaweza kusababisha maambukizi ya macho, maskio au hata tumbo.
Kuteleza bafuni nalo tatizo Ni dhahiri kwamba kuanguka bafuni kuna madhara mengi makubwa. Kwa kawaida sabuni na maji kwa pamoja huwa na tabia ya kuifanya sakafu kuwa ya kuteleza.
Sasa basi, watu huwa rahisi mno kuteleza bafuni na kuangukia sakafuni.
Wapo ambao wanaoanguka bafuni na kupata majeraha kwa kuvunjika mifupa, majeraha ya mwili na vidonda wanapoingia ama kutoka bafuni.
Ili kupunguza matatizo haya, wanashauriwa mazulia ya bafuni kwenye sakafu ambayo husaidia kuzuia kuteleza na kusafisha mabomba na sakafu za bafu mara baada ya kulitumia, hususan pale wanapotumia sabundi za mafuta (jeli) ama mafuta ya mwili.