STAA wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ni rasmi sasa amekuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo akifunga mabao 324 kwenye mechi 310.
Rekodi hiyo ameiweka juzi alipofunga bao moja wakati wakiilaza Levante mabao 3-0, mengine yakifungwa na Jesena Marcelo.
Tayari Real Madrid ilikuwa ikimtambua Ronaldo kuweka rekodi hiyo kabla ya mchezo huo, wakihesabia bao la faulo alilofunga dhidi ya Malmo mwaka 2010 lililombabatiza Pepe na kujaa wavuni, limeshampa tuzo ya kiatu mchezaji huyo, juzi alipewa tuzo rasmi.
Straika wa New York Cosmos, Raul Gonzalez, anayestaafu kucheza soka Novemba mwaka huu, ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid, lakini alitumia mechi 741 kufunga mabao 323.