Na Sheila Katikula, Mwanza
KLABU ya wakimbia riadha jijini Mwanza, RockCity runners wameamua kuanzisha mbio ili kuweza kupata pesa za matibabu kwa ajili ya watoto wenye ugonjwa wa usonji.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa mbio hizo Mwenyekiti wa klabu ya Rock City runners Kulwa Shimiyu alisema baada ya kuguswa kama wazazi imesababisha kuanzusha mbio hizo.
“Kutokana na shida wanazozipata watoto wetu wenye ugonjwa wa Usonji na matibabu yao yanahitaji gharama kubwa hivyo tunaamini kupitia mbio hizi tutapata pesa ambazo zitasaidia kupata matibabu watoto hawa wenye tatizo hili,” alisema.
Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Septemba 19 ambao zitakuwa ni mbio zikakazokimbiwa katika barabara za vumbi na milima yenye mawe ambapo kutakuwa na mbio za km 3.
Alisema ada ya ushiriki kwa watoto ni shilingi 35,000 kwa umbali wa km 8 na km 17 huku ada kwa wakubwa ni Sh 40,000 na pia kutakuwa na kifurushi kwa ajili ya familia kwa watu wawili mtoto na mzazi wake watalipa Sh 35,000.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Ilemela Hassan Masala alisema kuna baadhi ya watu hawatambui kama mtoto akipata usonji ana haki ya kulindwa kupendwa na kupata elimu kupitia mbio hizo watajufunza na kupelekea kuwathamini watoto hao.
“Sisi kama viongozi wa mkoa tumeguswa sana na mbio hizi kwani tunaamini watu wengi wahajui nini maana ya ugonjwa wa usonji, hivyo naamini kupitia mbio hizo watu wengi watafahamu kuhusiana na ugonjwa huu na mimi nitakuwa mshiriki namba moja,” amesema.
Masala amewaomba wazazi hususani wanaume kutokuwatelekeza wake zao na watoto hao kwani ni mipango ya Mungu kupata watoto wenye usonji kikubwa waatakiwa kishirikiana ili kuendesha malezi bora kwa mtoto wao.
“Tunafahamu ugumu wa kuwalea watoto hawa wenye usonji hivyo nawaomba wazazi haswa haswa akina baba wajitahidi kutokukwepa majukumu yao kwani tunaamini mtoto anatoka kwa Mungu hivyo tupokee kwa furaha hata kama mtoto hayuko sawa,” amesema Masala.