26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Riyama: Watu wamekosa hofu ya Mungu

Riyama-AliNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
MSANII wa filamu nchini, Riyama Ally, amewataka Watanzania kuwa na hofu ya Mungu na kuacha kuwadhulumu uhai wao walemavu wa ngozi ‘albino’.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Riyama alisema inashangaza watu ambao wamekuwa wakiendekeza imani za kishirikina, kwani wengi wao hushia pabaya na kukosa mafanikio.
Alisema imani potofu zimekuwa zikizidisha maovu hayo, huku baadhi ya watu wakijinufaisha wao bila kuangalia maisha ya wenzao.
“Watu hawana hofu ya Mungu kabisa, wamekuwa wakatili sana, wanashindwa kutambua kuwa albino ni binadamu wa kawaida,” alisema Riyama.
Alisema jamii inapaswa kuamka na kusimama kwa pamoja, kuwatetea albino ili kupunguza vifo na kuwapa maisha ya amani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles