Na Asha Bani, Dar es Salaam
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umewataka wananchi kuendelea kujitokeza na kuandika Wosia ili kujiepusha na migogoro ya mirathi inayotokea mara kwa mara katika familia.
Hayo yalielezwa jana na Afisa Mawasiliano wa RITA, Grace Kyasi katika viwanja vya Mnazi mmoja kunapoendelea maadhimisho siku ya sheria nchini.
Grace amesema kuandika Wosia kuna umuhimu wake huku akiwataka watanzania kuacha mawazo potofu juu ya kuandika wosia ambapo alisema wengi wao wamekuwa wakiamini kufanya hivyo ni sawa na kujichulia kifo cha mapema jambo ambalo halina ukweli.
Alisema kitendo cha kuandika Wosia suala la kisheria na lenye faida kubwa linapokuja suala la kusimamia Mirathi ya familia.
Pia RITA wamewataka wananchi kufika katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa ajili ya kupata vyeti vya kuzaliwa kwa ambao hawana,kuandika wosia na masuala ya udhamini
Amesema vyeti vya kuzaliwa vina matumizi makubwa na ya umuhimu yakiwemo kusaidia kwenye masuala ya ajira, vitambulisho vya utaifa na hata mikopo vyuoni hasa kwa wanafunzi.