29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

RITA yahimiza Watanzani kuchangamkia fursa ya Sabasaba

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Watanzania zaidi ya 3,000 waliotembelea banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) wamesajiliwa kwenye mfumo ambapo kati yao zaidi ya 2,000 tayari wamepatiwa vyeti vya kuzaliwa.

Hayo yamebainishwa Julai 9, jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Frank Kanyusi alipokuwa akishuhudia wananchi waliyojitokeza kwenye banda hilo ambalo lipo kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasana yanayoendelea.

“Tunatoa huduma zetu zote na tunaomba Watanzania wazidi kujitokeza kwa wingi maana tumejipanga vizuri kuwahudumia, tunatoa vyeti hapa hapa kwenye maonesho na tayari wananchi zaidi ya elfu mbili tumewapatia vyeti na tunatarajia wazidi kujitokeza ili wasipitwe na fursa hii,” amsema Kanyusi.

Amesema jumuku la RITA ni kutoa huduma bora kwa wananchi wake hasa ikiwemo cheti cha kuzaliwa kupitia maonesho hayo, elimu kuhusu mirathi, kuandika na kuhifadhi wosia na wametumia nafasi hiyo kuwasaidia Watanzania waweze kusaidiwa kwa haraka kupata cheti na urahisi kupata cheti cha kuzaliwa.

Aidha, baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma mbali mbali wamesifu utendajii kazi wa RITA na jitihada walizofanya kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa ndani ya siku moja.

“Tunawapongeza maana siyo kazi rahisi kuwahudumia watu wengi kiasi hiki, hii inaonyesha namn walivyojipanga vizuri, mimi nimejiandikisha na mepata cheti,” amesema Esther John.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles