28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

‘Ripoti za CAG ziendelee kujadiliwa bungeni’

Ludovick Utouh
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh

Na Mwandishi Wetu

MKAGUZI Mkazi wa Hesabu katika Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mkoa wa Arusha, Omary Mussa, amesema ipo haja ripoti ya CAG iendelee kujadiliwa bungeni.

Amesema hatua yaripoti hiyo kutojadiliwa bungeni kama ilivyokuwa awali inawanyima haki wananchi wanaotaka kujua namna fedha zao zinavyotumika katika taasisi mbalimbali nchini.

Musa alitoa wito huo jana alipokuwa akizungumza na MTANZANIA kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

“Hili suala la ripoti ya CAG kutojadiliwa bungeni mimi naona halikuwa sahihi kwa sababu wananchi wanataka kujua jinsi fedha zao zinavyotumiwa katika maeneo yao.

“CAG anapomaliza kukagua hesabu za fedha fulani kisha wabunge wakazijadili bungeni, wananchi wanapata fursa ya kujua ubadhirifu unavyofanyika na pia watajua jinsi Serikali ilivyochukua hatua kwani baada ya ripoti kujadiliwa Serikali nayo hutoa majibu ya kilichojadiliwa.

“Kwa maana hiyo, mimi nashauri kama inawezekana utaratibu huo uendelee yaani wabunge waendelee kujadili ripoti za CAG kama ilivyokuwa ikifanyika zamani,” alisema Mussa.

Kuhusu maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea, alisema kuna haja wananchi wakajitokeza kwa wingi katika banda lao kwani wataelezwa majukumu mbalimbali ya ofisi yao.

“Wananchi waje tu kwa wingi kwa sababu hapa tumejipanga, wakija tutawaeleza majukumu yetu katika ukaguzi wa hesabu na namna tunavyofanya kazi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles