28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Rihanna amuongezea umaarufu Flaviana Matata

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Mwanamitindo wa Kimataifa kutokea Tanzania anayefanya shughuli zake jijini New York, Marekani, Flaviana Matata, anagonga vichwa vya habari mara baada ya Mwimbaji maarufu duniani, Rihanna kum-follow kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwaka 2013 Flaviana alitajwa na Jarida la Forbes Africa kuwa ni miongoni mwa Wanamitindo wanaolipwa fedha nyingi zaidi, huku mwaka 2017 akitajwa na Okay.com kuwa miongoni mwa wanawake 100 bora Afrika.

Rihanna toka Marekani ana followers zaidi ya milioni 109, huku Flaviana akiwa nao milioni 1.7 kwenye mtandao huo ulioanzishwa Oktoba 2010 na sasa unamilikiwa na kampuni ya Facebook.

Katika kazi yake ya mitindo Flaviana amefanikiwa kusafiri katika nchi mbalimbali na kukutana na mastaa wakubwa kama Jay Z na mkewe, Beyonce.

Hadi sasa Flaviana amefanikiwa kutunukiwa tuzo kama Arise Fashion Magazine Awards (2011), Nigeria Next Super Model Awards (2012), Africa Diaspora Awards (2012), Swahili Fashion Week Awards (2012), Malkia wa Nguvu Awards (206) na Global Woman Gala (2018).

Mrembo huyo ambaye mwaka 2007 alishinda taji la Miss Universe Tanzania, kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation (FMF) amekuwa akitoa misaada ya vifaa na ada hasa kwa wanafunzi wa kike nchini Tanzania.

Flaviana Matata Foundation ilizinduliwa Juni 2011 ikiwa na lengo la kuanzisha mfuko wa kusaidia elimu ya watoto waishio katika mazingira magumu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles