29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Riba kubwa zatajwa kuwanyima fursa wananchi

Dorothy Mwanyika
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dorothy Mwanyika

Na Joseph Lino, DAR ES SALAAM

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dorothy Mwanyika, amesema wananchi wengi wanashindwa kutumia huduma za kibenki kutokana na makato ya huduma za fedha.

Mwanyika alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam wakati akizindua akaunti maalumu ya Kikundi ya Benki ya  Access Tanzania.

Alisema huduma za bure zinasaidia watu ambao hawana vigezo vya kupata mikopo kwenye benki nyingine.

“Kama inavyojulikana, vikundi vingi vilivyopo vijijini hupata wakati mgumu hasa kwenye kufikiwa na huduma za fedha kutokana na maeneo waliyopo, hivyo kupelekea kutumia njia za zamani ikiwamo kibubu kama njia ya kuhifadhi fedha.

“Nina hakika kupitia akaunti hii ya Kikundi, huduma za kibenki za bure zitawezesha wananchi wa kawaida kwa kupitia Access mobile kupata huduma za fedha.

“Huduma ya akaunti ya Kikundi ni mahsusi kwa ajili ya vikundi mbalimbali visivyo rasmi kwa kuweka akiba na kukopa vinavyojiwekea akiba kwa njia mbalimbali ili kukopeshana baadaye na inawezesha kwa kushirikaiana na Shirika la Care na Selcom,” alisema.

Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Access, Andrea Ottina, alisema akaunti hii inatoa simu tatu kwa wanachama wa kikundi husika ili kuhakikisha usalama wa fedha zao  na kufanya miamala kwa njia ya simu kwa niaba ya kikundi.

“Akaunti hii itaviwezesha vikundi kuendelea na shuguli zao bila kuvuruga ratiba zao za kila siku kwa sababu kila kitu hufanyika kupitia simu zao za mkononi,” alisema Ottina.

Mwakilishi kutoka Care International, Christian Pennotti, alisema wanasimamia vikundi 10,000 vyenye wanachama 250,000 vinavyohitaji huduma za kibenki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles