25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

RC Makonda aupongeza uongozi NCAA kwa malengo ya kukuza utalii

Na Mwandishi Wetu, NCAA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa kuweka malengo makubwa ya kukuza utalii na kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea eneo hilo kwa mwaka ujao 2025.

Mhe. Makonda ameeleza kuwa juhudi zilizowekwa na NCAA za kutangaza utalii, kuboresha miundombinu ya utalii, kujenga huduma za malazi na mafunzo kwa watumishi wanaohudumia wageni ziende sambamba na ushirikishwaji wa wananchi wa mkoa wa Arusha ambao ni wadau muhimu wa kujua vivutio vilivyopo ili wanapokutana na wageni katika maeneo mbalimbali wawe na uwezo kuelezea fursa za utalii zilizoko mkoa wa Arusha.

“Mikakati mliyonayo ni ya kupongezwa, mwaka uliopita mlifikisha wageni takribani 752,000, naamini mwaka huu mtavuka zaidi, mikakati mliyoiweka ni tafsiri ya vitendo na maono ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kuitangaza nchi yetu kupitia filamu ya Tanzania the Royal tour , sasa naomba utekelezaji wa mipango hii kwa kila hatua kuwe na ushirikishwaji na elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha, Serikali ya Mkoa na Wilaya ya Karatu” aliongeza Mhe. Makonda.

Akitoa taarifa ya mendeleo ya utalii katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi NCAA Vicktoria Shayo ameeleza kuwa idadi ya wageni imeendelea kuongezeka ambapo kati ya Julai 2023 hadi aprili, 2024 jumla ya wageni 780,281 wameshatembelea eneo la hifadhi Ngorongoro.

Kamishna Shayo amebainisha kuwa kwa sasa Serikali kupitia NCAA inaendelea kuboresha shughuli za uhifadhi na kuboresha maendeleo ya wananchi ikiwemo kuboresha huduma bora zaidi za kijamii nje ya hifadhi hasa katika Kijiji cha Msomera, Kitwai na Saunyi ambapo Serikali inaendelea kujenga nyumba za makazi na miundombinu mingine ya kijamii kwa ajili ya wananchi wanaoendelea kujiandikisha kuhama kwa hiari.

Katika hatua nyingine Mhe. Makonda ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la makao Makuu ya NCAA Karatu Mkoani Arusha ambapo ujenzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kupunguza shughuli za binadamu ndani ya Hifadhi ili kuboresha uhifadhi na kuboresha maisha ya wananchi wa Ngorongoro na kuwajengea miundombinu bora ya kijamii nje ya Hifadhi.

Akitoa taarifa za ujenzi wa jengo hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi huduma za Uhandisi NCAA Mhandisi Daniel Chegere amesema ujenzi huo katika awamu ya kwanza unahusisha Jengo la ofisi za makao makuu na nyumba tatu za viongozi wakuu wa shirika ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 80 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles